• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 7:50 AM
Uhuru, Raila wasema Azimio ni mwanzo mpya Kenya

Uhuru, Raila wasema Azimio ni mwanzo mpya Kenya

Na BENSON MATHEKA

RAIS Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga wametaja muungano mkubwa wa kisiasa wanaounda wa Azimio la Umoja kama utakaoleta pamoja mwanzo mpya na kuandika upya historia ya Kenya.

Viongozi hao walisema kwamba wanataka kuona Wakenya wakiishi kwa amani kama taifa moja kuelekea na baada ya uchaguzi mkuu ujao.

Wakihutubia makongamano ya kitaifa ya vyama vyao vya Jubilee na ODM, wawili hao walisema kwamba nia yao ni kuepuka migawanyiko ya kikabila na kisiasa inayosababisha ghasia kila baada ya miaka mitano.

“Jinsi mnavyotuona hapa, huu ni mwanzo mpya katika nchi yetu,” Rais Kenyatta alisema.

Akihutubia wajumbe wa kitaifa wa chama cha ODM, kabla ya kuelekea KICC kuhudhuria lile la Jubilee, Bw Odinga alisema historia ya Kenya inaandikwa upya chini ya Azimio la Umoja.

Walisema wana hakika kwamba muungano huo utashinda uchaguzi mkuu ujao.

“Tumeanza safari mpya katika nchi yetu, tunataka kurekebisha makosa ya awali ambayo yamekuwa jinamizi katika nchi yetu na kunyima watu wetu nafasi ya kufurahia mazuri ya nchi yao kama nchi iliyoungana,” akasema Bw Odinga.

  • Tags

You can share this post!

Msilazimishe vyama vidogo kuungana – Muturi

Yafichuka daraja la OKA na Azimio ni Gideon Moi

T L