• Nairobi
  • Last Updated December 2nd, 2023 1:45 PM
Yafichuka daraja la OKA na Azimio ni Gideon Moi

Yafichuka daraja la OKA na Azimio ni Gideon Moi

Na BENSON MATHEKA

MWENYEKITI wa chama cha Kanu Gideon Moi ndiye daraja lililounganisha muungano wa One Kenya Alliance OKA na Azimio la Umoja linaloongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga.

Hayo yalifichuliwa Jumamosi kwenye kongamano la kitaifa la chama cha Jubilee mmoja wa vinara wa OKA, Bw Cyrus Jirongo, alipompongeza Bw Moi kwa kuleta pamoja mirengo hiyo miwili.

“Namshukuru sana Bw Gideon Moi kwa kuwa uliweza kuleta wanaume hawa pamoja,” Bw Jirongo alisema.

Bw Moi na kinara mwingine wa OKA, Kalonzo Musyoka wa Wiper walihudhuria kongamano hilo katika uwanja wa Kenyatta International Conference Center Nairobi.

Akizungumza katika kongamano la kitaifa la wajumbe wa Jubilee, mbele ya vinara hao, Bw Odinga na Rais Uhuru Kenyatta, kiongozi chama cha Narc Charity Ngilu alisema kwamba haikuwa rahisi kuwaleta pamoja vigogo hao wa kisiasa waliokuwa na misimamo mikali hasa Bw Musyoka aliyekuwa ameapa kuwa angemuunga Bw Odinga kwa mara ya tatu.

Bw Moi alisema kwamba nia ya OKA kuungana na Azimio ni kuleta umoja na uwiano nchini.

You can share this post!

Uhuru, Raila wasema Azimio ni mwanzo mpya Kenya

Liverpool, Chelsea fataki zitafyatuka

T L