• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
Utata Pwani Wiper ikimpa Sonko tikiti ya moja kwa moja

Utata Pwani Wiper ikimpa Sonko tikiti ya moja kwa moja

NA WINNIE ATIENO

SIKU chache baada ya chama cha Wiper kumpa tikiti ya moja kwa moja Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo anayegombea kiti cha ugavana Kaunti ya Mombasa, mgawanyiko umeibuka kwenye chama hiyo.

Hii ni baada ya chama hicho kumpa aliyekwua gavana wa Nairobi Mike Sonko tikiti ya Wiper kugombea ugavana wa Mombasa.

Wakuu wa chama hicho wakiongozwa na Bi Agatha Solitei ambaye ni naibu mwenyekiti wa bodi ya kitaifa ya uchaguzi walidinda kuzungumza na Taifa Leo.

Bi Solitei aliiambia Taifa Leo kuandika ujumbe mfupi kwani hangeweza kuongea. Hata hivyo hakujibu maswali ya mwandishi huyu yanayohusiana na tikiti hiyo.

“Maswali yanayoibuka ni kwamba chama hicho kitafanya mchujo? Kwa nini Bw Mbogo alipewa tikiti ya moja kwa moja? Mbona tena Sonko akapewa tikiti baada ya Bw Mbogo.” Lakini Bi Solitei hakujibu maswali hayo.

Bw Mbogo naye hakupatikana kwenye simu yake ya rununu. Bw Sonko alijiunga na Wiper hivi majuzi. Hata hivyo, wandani wake walisema kwamba atatoa taarifa kamili kuhusu tikiti hiyo baadaye.

Baada ya kupewa tikiti ya moja kwa moja Bw Mbogo alipata afueni akisema tikiti hiyo imempa motisha na msukumo wa kukomboa wakazi wa Mombasa kutokana na uongozi mbaya.

Alisema ana matumaini ya kushinda uchaguzi wa ugavana kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

“Nilihudhuria mkutano wa wagombea wa chama cha Wiper jijini Nairobi ambako nilitunukiwa tikiti ya moja kwa moja sababu sikuwa na mpizani kwenye chama chetu. Nimeshahitimu

sasa ni kwenda uwanjani kusaka kura,” alisema Bw Mbogo.

Mbunge huyo ambaye amekuwa akikosoa uongozi wa Gavana Joho atamenyana na Hassan Omar (UDA), naibu wa gavana wa Mombasa Dkt William Kingi wa Pamoja African Alliance (PAA) na mwaniaji wa ODM.

ODM haijatangaza kiongozi atakayepeperusha bendera ya chama chake huku mdahalo wa kumsaka ukiendelea. Mbunge wa Mvita Bw Abdulswamad Nassir na mfanyabiashara, Suleiman Shahbal wanamenyania tikiti ya ODM.

  • Tags

You can share this post!

Jicho kisoka lalenga Sergio Ramos wa PSG

Pasaka: Hoteli zafurika

T L