• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 8:46 PM
Vuguvugu labuniwa ‘kumkata miguu’ Raila ngomeni Nyanza

Vuguvugu labuniwa ‘kumkata miguu’ Raila ngomeni Nyanza

NA JUSTUS OCHIENG

KIONGOZI wa Azimio la Umoja, Bw Raila Odinga, anakabiliwa na uasi mpya katika ngome yake ya Nyanza, baada ya wabunge wanaodaiwa kuwa waasi kubuni ‘vuguvugu la ukombozi’ kuvuruga ushawishi wake kwa usaidizi wa utawala wa Rais William Ruto.

Tayari, imebainika kuwa jina la vuguvugu hilo limebuniwa ili kuonyesha mipango ya ‘kulikomboa’ eneo hilo kutoka kwa ushawishi wa Bw Odinga ambao umedumu tangu uhuru wakati babake, Jaramogi Oginga Odinga, alikuwa kiongozi wa kisiasa wa jamii ya Waluo.

Rais Ruto amekuwa akiwafikia wabunge kutoka upinzani lengo lake kuu likiwa kupunguza ushawishi wa Bw Odinga. Hii ni licha ya Bw Odinga kutoa miito kwa wabunge hao kupinga utawala wa Rais Ruto.

Vuguvugu hilo linadaiwa kuongozwa na mbunge Gideon Ochanda (Bondo) huku katibu wake akiwa mbunge Felix Odiwuor maarufu kama ‘Jalang’o’ (Lang’ata).

Rais tayari amefanya mazungumzo na wabunge wa chama cha Jubilee chake Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta ambapo amefaulu kuwashawishi baadhi yao kujiunga naye.

Pia, anafanya mazungumzo na baadhi ya wabunge wa ODM kutoka Nyanza ambao Bw Odinga amewataja kuwa “waasi” wasio pamoja naye kwenye harakati za ukombozi.


  • Tags

You can share this post!

Mwanafunzi asuka makuti akisaka karo kuingia shule ya upili

Wataangukia kitu serikalini?

T L