• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:55 AM
Wandani wa Raila wapiga jeki kampeni za Natembeya

Wandani wa Raila wapiga jeki kampeni za Natembeya

NA GERALD BWISA

AZMA ya aliyekuwa Kamishna wa Ukanda wa Bonde la Ufa, Bw George Natambeya ya kusaka ugavana wa Trans Nzoia imepigwa jeki baada ya kuungwa mkono na washirika wa kinara wa ODM, Bw Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta.

Hapo jana Jumamosi, Waziri wa Kilimo, Bw Peter Munya, Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa, Gavana wa Mombasa Hassan Joho, Wycliffe Wangamati wa Bungoma na Lee Kinyanjui (Nakuru) waliahidi kumpigia kampeni kali Bw Natembeya kuhakikisha anatwaa wadhifa huo.

Viongozi hao walikuwa wakizungumza katika uwanja wa Kenyatta mjini Kitale katika hafla ya kumlaki Bw Natembeya nyumbani, wiki tatu baada ya kustaafu.

Muda wa watumishi wa umma wanaomezea mate nyadhifa za uongozi kujiondoa afisini ni Februari 9.

“Tumechagua ‘farasi’ wa Azimio kwa sababu tunaunganisha Wakenya lakini wenzetu wanahubiri injili ya mgawanyiko. Muungano wa Kenya Kwanza hauna manufaa yoyote na wasije hapa Kitale kutugawa kwa makabila,” akasema Bw Wamalwa.

Bw Natembeya ambaye atawania kiti hicho chini ya Chama kipya cha DAP-K aliahidi kujenga upya uwanja huo wa kihistoria na pia kuongoza vyema kwa kuwatendekea kazi watu wa Trans Nzoia kazi kwa dhati.

“Kuanzia mwezi wa tisa raia atakuwa mbele na afisa wa serikali nyuma. Hata kabla hamjanichagua, nitaongea na Rais ili ajenge upya uga huu kuondoa aibu hii wageni wetu wanaona,” akasema Bw Natembeya huku akishangiliwa na raia waliojaa uwanjani humo.

  • Tags

You can share this post!

Raila na Ruto wararuana vikali Mlimani

Karua ajiunga na OKA akiahidi kutumikia nchi vyema...

T L