• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 3:10 PM
Wakazi wang’angania mahindi baada ya watu 4 kuangamia ajalini

Wakazi wang’angania mahindi baada ya watu 4 kuangamia ajalini

NA MAGDALENE WANJA

WAKAZI Kaunti ya Nakuru Jumatatu waling’ang’ania mahindi baada ya ajali iliyosababisha vifo vya watu wanne kutokea katika eneo la Eveready kwenye barabara kuu ya Nakuru kuelekea mjini Eldoret. Kati ya wanne hao, wawili walikuwa wafanyakazi wa gereza.  

Ajali hiyo iliyotokea mchana ilihusisha magari manne, lori la gereza, trela la mafuta, matatu na lori lililokuwa linasafirisha mahindi, iliacha zaidi ya watu 20 wakiuguza majeraha.

Kwa mujibu ya walioshuhudia ajali hio, lori la magereza ya Kenya lilikuwa likielekea mjini Nakuru kabla ya dereva kupoteza udhibiti katika daraja la Soilo na kugongana na matatu.

Lori hilo halikusimama hadi lilipofika eneo la Eveready, baada ya kilomita moja ambapo lilligongana na lori la mafuta.

Wakazi waliokusanyika kwenye eneo hilo walionekana waking’ang’ania mahindi yaliyomwagika barabarani baada ya ajali.

Wakazi wakipakia mahindi kwa mifuko kwenye eneo la ajali Septemba 24, 2018. Picha/ Maggy Wanja

“Lori liligongana na matatu karibu na daraja la Soilo lakini halikusimama. Liliendelea kwa kasi na kugongana na magari hayo mengine “, alisema Stephen Mwaura, aliyeshuhudia kisa hicho.

Afisa wa Trafiki, Bw Zero Arome alithibitisha ajali hiyo ya kipekee iliyohusisha magari manne.

Afisa wa Hospitali ya Nakuru Level 5 Bw Alphaxard Kemboi alisema wamepokea majeruhi 22 kutokana na ajali hiyo.

You can share this post!

Bondia Anthony Joshua azoa Sh2 bilioni kwa kumlima Povetkin

Orodha ya wanaowania tuzo za FIFA

adminleo