• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 9:50 AM
Masharti makali yanayomkabili Obado

Masharti makali yanayomkabili Obado

Na CECIL ODONGO

INGAWA Gavana wa Migori Okoth Obado sasa anasababu ya kutabasamu baada ya kuachiliwa kwa dhamana ya Sh5 milioni na mahakama kuu ya Nairobi kutokana na kesi ya mauaji ya Sharon Otieno iliyokuwa ikimkabili, mtihani mkubwa kwake hata hivyo utakuwa jinsi atakavyokabiliana na masharti makali aliyowekewa na jaji huyo.

Jaji Jessy Lessit Jumatano Oktoba 24 alimwekea gavana huyo masharti saba makali na kusema kwamba hatasita kumtia mbaroni na kuzuiliwa iwapo atayakiuka.

Masharti hayo ni gavana kutoweza kusafiri umbali wa kilomita 20 nje ya kaunti ya Migori, hawezi kutoa sababu zozote za kusitisha vikao vya kesi, lazima aripoti kwa naibu msajili wa mahakama mara moja kila mwezi na hawezi kujadili maswala yanayohusiana na kesi hiyo katika mikutano ya kisaiasa.

Mengine ni kuzuiwa kutishia wazazi na jamaa wa marehemu Sharon Otieno, kutoa pasipoti na stakabadhi nyingine za usafiri ili yawekwe mahakamani na kutotoa vitisho kwa mashahidi katika kesi hiyo.

Kesi hiyo itatajwa Februari 14, 2019 kisha isikizwe Mei 6, 2019.

You can share this post!

Juhudi za kuimarisha chakula cha kutosha nchini zaongezeka

Chiloba kuitwa bungeni kujibu maswali licha ya kupigwa...

adminleo