• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 10:50 AM
UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Chimbuko na sababu za kutumia misimu katika jamii (Sehemu ya Pili)

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Chimbuko na sababu za kutumia misimu katika jamii (Sehemu ya Pili)

Na MARY WANGARI

MISIMU hutumiwa kwa ajili ya kutaka mazungumzo yawe siri; yasieleweke kwa watu wengine.

Hutumiwa ili kufanya mambo mazito kuwa mepesi. Kwa mfano, mtua napokusaidia kutenda jambo na atake kuhongwa anaweza kukuuliza,‘ hata chai?’ badala ya kukuuliza,’’ mbona hunipi hongo?’’

Pia ipo dhana potovu kuwa matumizi ya misimu ndiyo ujuzi wa lugha.

Sababu nyingine ni kutojua lugha moja vizuri. Kwa mfano, wasemaji wengi hawajui Kiswahili wala Kiingereza vyema hivyo wanaamua kutumia misimu.

Hutumika kama uraibu kwa vijana.

Misimu hurahisisha mawasiliano. Maneno ya misimu hueleweka kwa haraka, hasa yanapotumika badala ya maelezo mengi.

Hutumiwa kama tauria au tasfida. Kuna baadhi ya misimu ambayo hupunguza ukali wa maneno hasa lugha ile inayoonekana ya matusi. Kwa mfano: kukeketa mabinti badala ya kutahiri mabinti.

Misimu huunganisha watu. Watu wa tabaka mbalimbali wanapokuwa katika mazungumzo huelewana vyema wanapotumia lugha wanayofahamiana.

Baadhi ya misimu huikosoa na kuiasa jamii. Misimu ya namna hii huwa na hisia za kejeli, bezo, dhihaka, chuki na kusifu kusiko kwa kawaida.

Misimu huibua hisia za wazungumzaji na hata wasikilizaji. Aghalabu misimu hubeba hisia za furaha, huzuni, chuki, mshangao, mzubao miongoni mwa hisia nyingine.

Misimu huibua hisia ya furaha na ucheshi. Hii ni kwa kwa sababu maneno ya misimu yana mvuto na kuwa na chuku yanapotumiwa na kuchekesha.

[email protected]

Marejeo

Mbaabu, I. (1996). Language Policy in East Africa: A Dependency Theory Perspective. Nairobi: Educational Research and Publications.

Masebo, J.A., Nyangwine A. D., (2002) Nadharia ya Lugha: Kiswahili 1. Dar es Salaam: Afroplus Industries Ltd.

Massamba, D.P.B. (2002). Historia ya Kiswahili 50 BK. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

You can share this post!

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Simo/ Misimu katika jamii...

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Nafasi ya lugha sanifu katika...

adminleo