• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 7:55 PM
Jinsi ya kujitengenezea chokoleti nyumbani

Jinsi ya kujitengenezea chokoleti nyumbani

Na MARGARET MAINA

[email protected]

UNAWEZA kutengeneza chokoleti ukiwa nyumbani kwa kutumia vifaa vya nyumbani na vitu kadhaa vinavyopatikana madukani.

Muda wa kuandaa: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika

· siagi kikombe kimoja

· cocoa powder kikombe 1

· icing sugar/sukari iliyosagwa au asali kikombe ½

· maji kikombe ½

· vanilla ya maji kijiko 1 cha chai

· chumvi

Maelekezo

Pima sukari na cocoa powder kwenye sufuria. Ongeza maji kwenye mchanganyiko wa sukari na poda ya cocoa.

Weka maji kwenye sufuria kubwa kwa ujazo wa robo kisha weka kwenye moto wa wastani.

Weka sufuria ya saizi ya kati iliyo na poda ya cocoa, sukari na maji juu ya sufuria kubwa (double boiler).

Wakati maji yaliyoko kwenye sufuria kubwa yanachemka, koroga mchanganyiko wako wa poda ya cocoa taratibu kwa muda wa robo saa mpaka iwe nyepesi kama uji.

Ondoa sufuria ya mchanganyiko wa chokoleti kwenye moto, kisha ongeza siagi iyeyukie, ongeza vanila.

Tumia blenda ili kufanya chokoleti iwe laini isiwe na mabuja.

Mimina mchanganyiko wa chokoleti kwenye ice cube tray halafu acha kwa muda wa dakika tano isawazike.

Weka ice cube tray iliyo na chokoleti kwenye jokovu, usiku kucha.

Chokoleti ikiwa tayari, toa tray, ondoa chokoleti kwenye tray tayari kwa kuliwa.

Furahia.

  • Tags

You can share this post!

Kitendawili cha barakoa

Walinzi na wafuasi wa Bobi Wine wakamatwa, siku mbili kabla...