• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Unayostahili kufanya ili kujikinga na ugonjwa wa moyo

Unayostahili kufanya ili kujikinga na ugonjwa wa moyo

Na MARGARET MAINA

[email protected]

WATU wengi hawana ufahamu wa vitu ambavyo huchangia pakubwa katika magonjwa yasiyoambukizana kama ugonjwa wa moyo, kisukari, msukumo wa damu na kadhalika.

Hivyo basi ili kujiepusha na magonjwa kama ugonjwa wa moyo ambao siku hizi huwapata watu wa rika zote, kiafya inashauriwa kila siku kufanya yafuatayo:

Epuka sigara

Uvutaji wa sigara huchangia kwa asilimia kubwa magonjwa ya moyo na kansa kutokana na moshi wenye kemikali unaoenda kuharibu mapafu, kifua na kufanya moyo kutanuka. Hivyo ni muhimu kuepuka uvutaji sigara ili kujiepusha na madhara hayo.

Tumia mvinyo wa zabibu angalau glasi moja

Ila kinywaji hii kitumiwe kwa kiwango maalumu kwani kiwango cha wastani cha pombe yenye kilevi husaidia kuyeyusha mafuta mwilini na kuufanya mwili uwe na kiwango kizuri cha mafuta. Mafuta mengi mwilini husababisha magonjwa ya moyo.

Punguza kiwango cha chumvi unayotumia

Kwa siku mtu anatakiwa kutumia kiasi kidogo cha chumvi kwa kutumia kipimo cha kijiko kidogo cha chai, kwani tafiti zimeonyesha kuwa watu wanaotumia kiwango kikubwa cha chumvi hudhurika na magonjwa ya moyo.

Inashauriwa kutumia chokoleti nyeusi

Kipande kimoja cha chokoleti kwa siku husaidia katika kuweka sawa afya ya moyo wako kutokana na virutubisho kisayansi vinavyojulikana kama Antioxidants na flavonoids.

Jizuie kutumia lifti, badala yake tumia ngazi

Ofisi nyingi ni ghorofa hivyo watumiaji wa ofisi hizo hupendelea kutumia lifti. Lakini madaktari wanashauri kwa afya ya moyo wako, ni vyema kutumia ngazi ili kuweka mapigo ya moyo wako sawa na kufanya mazoezi na kwa kufanya hivi si lazima kwenda mazoezini kwani kupanda ngazi ni zoezi tosha.

Zingatia matunzo bora ya kinywa chako

Tafiti mbalimbali zimebainisha kuwa matunzo mabovu ya kinywa yanahusiswha moja kwa moja na magonjwa ya moyo. Hivyo inashauriwa kusafisha kinywa mara kwa mara ili kuua bakteria na vijidudu vinavyotengenezwa kinywani.

  • Tags

You can share this post!

Shinikizo mbunge amlipe mpenzi wa zamani Sh200,000 kila...

Washtakiwa kulangua raia wa Burundi