• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
Washtakiwa kulangua raia wa Burundi

Washtakiwa kulangua raia wa Burundi

Na RICHARD MUNGUTI

WASHUKIWA wawili wa ulanguzi wa binadamu wamejipata motoni baada ya kushtakiwa katika Mahakama ya Milimani Nairobi.

Boniface Kanuku Muia na Dennis Malulu Mulandi walikana walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) wakiwa na raia wawili wa Burundi waliokuwa wanawasafirisha kinyume cha sheria.

Muia na Mulandi walishtakiwa kuwa mnamo Feburuari 19, 2021 katika uwanja wa JKIA walikamatwa na maafisa wa idara ya Uhamiaji wakiwa na wanawake wawili , raia wa Burundi.

Wawili hao  hakimu mkuu Bi Martha Mutuku alielezwa, walikuwa wamepiga stempu feki ya idara ya uhamiaji katika pasipoti za wanawake hao waliotambuliwa kwa herufi za majina yao HN na HM.

Bi Mutuku alijuzwa, washtakiwa walikuwa wameidhinisha kuwapo kwa walalamishi hao nchini Kenya kwa kupiga stempu feki katika pasipoti zao.

Muia na Mulandi walikana shtaka la kwanza la ulanguzi wa binadamu na pia kupiga stempu feki ya idara ya uhamiaji katika pasipoti za walalamishi.

Kiongozi wa mashtaka Bw Anderson Gikunda aliomba hakimu aamuru kesi hiyo iwasilishwe mbele ya korti itakayoisikiza Jumatatu saa nane unusu itengewe siku ya kusikizwa hivi punde kwa vile “wanawake hao wamezuiliwa katika makazi maalum.”

“Naomba kesi dhidi ya washtakiwa hawa itajwe mbele ya hakimu atakayeisikiza ndipo wahasiriwa wafike kortini. Kwa sasa wamezuiliwa katika makazi maalum,” Bw Gikunda alisema.

Hata hivyo , mahakama ilielezwa, ombi la washtakiwa kuachiliwa kwa dhamana halipingwi.

You can share this post!

Unayostahili kufanya ili kujikinga na ugonjwa wa moyo

Bale angali tegemeo kubwa kambini mwa Spurs – Mourinho