• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 8:50 AM
Kampuni za dawa zaonya wananchi dhidi ya chanjo feki ya corona

Kampuni za dawa zaonya wananchi dhidi ya chanjo feki ya corona

Na CHARLES WASONGA

CHAMA cha kampuni za kuuza dawa nchini (Pharmaceutical Society of Kenya-PSK) kimeonya watu binafsi dhidi ya kuuzia umma aina mbalimbali za chanjo ya Covid-19 kupitia mitendao ya kijamii.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Rais wa PSK Louis Machogu alitaja hatua hiyo kama inayokiuka maadili ya kitaaluma na inayokiuka kanuni zilizowekwa na Bodi ya Dawa na Sumu Nchini (KPPB).

“Mauzo yanayoendelea mitandaoni yanaweza kuchangia kuchipuka kwa sakata za uuzaji wa chanjo feki za Covid-19 nchini,” akasema Dkt Machogu.

Kinara huyo wa PSK pia aliwaonya Wakenya kuhuus biashara inayoendelea ulimwenguni ya kugushi aina maarufu za chanjo ya Covid-19 kama vile AstraZeneca kutoka India, Pfizer kutoka Amerikam na Sputnik V kutoka Urusi.

PSK imetoa wito kwa Wakenya, asasi za serikali na asasi za kusimamia dawa nchini kuwa macho na walinde masilahi ya umma.

“Hatutaki kuona wananchi wakipunjwa wakati huu ambapo uchumi wa nchini unakabiliwa na changamoto nyingi zinazosababishwa na janga hili la Covid-19,” akasema Dkt Machogu.

Taarifa ya PSK imejiri wakati ambapo baadhi ya Wakenya waliweka jumbe katika mtandao wa kijamii wa twitter wakisifia chanjo ya Sputnik V na kudharua ile ya AstraZeneca ambayo imedaiwa kusababisha madhara mwilini.

Bungeni, aliyekuwa kiongozi wa wengi Aden Duale aliwaambia wabunge wenzake kwamba hajapata chanjo ya Covid-19 lakini anapendelea chanjo ya Sputnik V.

“Nampongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kujitokeza juzi kupokea chanjo. Hatua hiyo imewapa Wakenya motisha na moyo wa kushirikisha shughuli hiyo muhimu. Kwa hivyo, natoa wito kwa serikali kuagiza chanjo zaidi ili Wakenya wengine waweze kufaidi. Mimi pia nitajitokeza kuchanjwa lakini napendelea chanjo hii kutoka Urusi kwa jina, Sputnik V,” Daule ambaye ni Mbunge wa Garissa Mjini akasema alipokuwa akichangia mjadala kuhusu kuahirishwa kwa vikao vya bunge kuzuia msambao wa corona.

You can share this post!

Ninafurahia BBI imesambaratika, tuliomba Mungu sana –...

Kamatakamata ya wasiovalia maski yafika mitaani