• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 2:25 PM
UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Jinsi ya kuandaa ratiba ya kudurusu nyumbani na umuhimu wake

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Jinsi ya kuandaa ratiba ya kudurusu nyumbani na umuhimu wake

Na MARY WANGARI

MASOMO kama vile Hisabati, Fizikia, Kemia na Bayolojia huhitaji kufanyiwa mazoezi ya mara kwa mara kuhusu fomula na kanuni kuu muhimu hivyo basi hakikisha unatenga muda wa kutosha ili kufanya mazoezi ya kutosha.

Wakati – Panga masomo kwenye ratiba yako kwa kuzingatia uzito wa somo husika.

Masomo ya sayansi kama vile Hisabati, Fizikia, Biolojia na Kemia kwa mfano huhitaji mwanafunzi kuzamia na kutumia akili zaidi ili kuelewa vipengele na kanuni fulani.

Hivyo basi, unaweza kulitengea muda kabla ya kufanya lolote wakati akili bado hazijachoka kwa kudurusu.

Unaweza pia ukatenga muda kwenye ratiba yako baada ya kumaliza kudurusu masomo kadhaa uliyotenga kwa siku hiyo, na kufanya maswali kadhaa ya somo kama hisabati kila siku.

Mtindo wa maisha – Hakikisha unapanga na kuunda ratiba yako ukiwa umetulia pasipo shinikizo lolote ili uweze kupata matokeo bora.

Tilia maanani mtindo wa maisha wa mwanafunzi husika unapotenga muda wa masomo ya siku kwenye ratiba ya nyumbani.

Kuna tofauti kuu ya mpangilio wa masomo kwa mwanafunzi wa shule ya bweni na mwanafunzi wa kutwa ambayo haiwezi kupuuzwa.

Wanafunzi wa kutwa aghalabu hulazimika kuamka mapema alfajiri kujiandaa na kuanza safari kuelekea shuleni ambapo wakati muhimu hupotezwa katika safari ya kuelekea shule asubuhi na kurejea nyumbani magharibi.

Hata anapowasili nyumbani, mwanafunzi wa kutwa kando na majukumu ya kinyumbani yanayomsubiri, aghalabu huwa amechoka ikizingatiwa anatarajiwa kurauka alfajiri itakayofuata na kuendelea na mkondo huo hadi mwisho wa juma.

Japo atajizatiti na kudurusu, si ajabu kumpata mwanafunzi kama huyo akisahau yote aliyosoma au kushindwa kuelewa hata baada ya kudurusu.

Mwanafunzi kama huyo anapaswa kutumia vyema kipindi cha likizo na kuhakikisha ana muda wa kutosha wa kupumzika na kudurusu akiwa ametuliza akili na kumakinika.

Insha – Unapoandaa ratiba ya nyumbani, tenga muda pia wa kuandika insha mara kwa mara kuhusu mada mbalimbali na kumpa mwalimu wako wa Kiswahili asahihishe na kukukosoa.

Hii itamsaidia mwanafunzi kupata makali ya uandishi wa insha mbalimbali ambazo anaweza kutahiniwa nazo pamoja na kuboresha matumizi yake ya lugha.

Zingatia vilevile katika ratibu yako masomo mengine kama vile Sayansi Jamii, Somo la Dini, Historia, Jiografia na kadhalika.

[email protected]

You can share this post!

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Ratiba ya kudurusu nyumbani kwa...

Sheffield United yaduwaza Brighton katika gozi la EPL