• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
SHAIRI: Kaozwa mapema bila ujuzi

SHAIRI: Kaozwa mapema bila ujuzi

NA ASSUMPTA WAUSI

Niketipo nina haya ,yanisakama maizi

Kaozwa pasi na haya ,mtoto bila ujuzi

Ilikuwa ja ruiya ,kakatiziwa ulezi

Mtima una kilio,huku kazi kazi kazi .

 

Mi mtoto kama yaya ,watoto ninao zizi

Niko nyumbani kuleya ,nguvu ninazo tukizi

Nipitiayo hekaya ,kapatwa nayo machozi

Mtima una kilio ,huku kazi kazi kazi .

 

Nionapo wa ulaya ,wenzangu wana mizizi

Wako na bashasha ghaya ,mwenzenu kwa usingizi

Elimu yao kamwaya ,mwangaza si kama juzi

Mtima una kilio ,huku kazi kazi kazi .

 

Bukrata wa ashiya ,mbuzi ,ng’ombe zote hizi

Msimu wa gonjwa baya, baridi sina malazi

Kuozwa kweli kinaya ,mapema kama ndizi

Mtima una kilio ,huku kazi kazi kazi.

 

#GirlChildVoice

You can share this post!

MWANAMUME KAMILI: Mume kamili hawezi kumtoa uhai mkewe

Mahanga adhihirisha uaminifu wa dhati kwa Obado