• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Chelsea waweka Fulham katika hatari ya kuteremshwa ngazi kwenye EPL

Chelsea waweka Fulham katika hatari ya kuteremshwa ngazi kwenye EPL

Na MASHIRIKA

KAI Havertz alifunga mabao mawili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Fulham na kuimarisha nafasi ya Chelsea katika nafasi ya nne kadri wanavyofukuzia fursa ya kushiriki soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao wa 2021-22.

Matokeo hayo yaliwaweka Fulham ya kocha Scott Parker katika hatari zaidi ya kuteremshwa kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu.

Havertz aliwafungulia waajiri wake ukurasa wa mabao katika dakika ya 10 baada ya kushirikiana na fowadi Mason Mount. Goli la pili ambalo Havertz alipachika wavuni mwanzoni mwa kipindi cha pili lilikuwa zao la ushirikiano mkubwa kati yake na Timo Werner.

Ingawa Fulham walijituma zaidi katika kipindi cha pili, makombora ya wanasoka Antonee Robinson na Ola Aina yalidhibitiwa vilivyo na kipa wa Chelsea, Edouard Mendy.

Zikisalia mechi nne pekee kwa kampeni za EPL msimu huu kutamatika rasmi, Fulham wanahitaji alama tisa zaidi ili kujiondoa ndani ya mduara unaojumuisha vikosi vitatu vya mwisho jedwalini.

Ushindi wa Chelsea unatarajiwa sasa kuwapa motisha zaidi kadri wanavyojiandaa kurudiana na Real Madrid kwenye nusu-fainali ya UEFA mnamo Mei 5, 2021 ugani Stamford Bridge.

Chini ya mkufunzi Thomas Tuchel, Chelsea watahitaji kusajili angalau sare tasa ili kutinga fainali itakayowakutanisha ama na Manchester City au Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa.

Baada ya kuvaana na Real, Chelsea watakutana na Man-City katika gozi la EPL uwanjani Etihad. Fulham kwa upande wao wana siku tisa za kupumzika kabla ya kualika Burnley mnamo Mei 10, 2021 ugani Craven Cottage kwa ajili ya kivumbi cha EPL.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Atletico wacharaza Elche na kunusia ubingwa wa La Liga

Neymar awabeba PSG dhidi ya Lens na kuendeleza presha kwa...