• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 6:55 PM
Neymar awabeba PSG dhidi ya Lens na kuendeleza presha kwa viongozi wa jedwali Lille

Neymar awabeba PSG dhidi ya Lens na kuendeleza presha kwa viongozi wa jedwali Lille

Na MASHIRIKA

NEYMAR alifunga bao na kuchangia jingine katika ushindi wa 2-1 waliousajili dhidi ya Lens katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) mnamo Jumamosi.

Ushindi huo uliwawezesha PSG kukalia kileleni mwa jedwali kwa muda mfupi kabla ya kupitwa tena na Lille waliowakung’uta Nice 2-0 na kusalia wakihitaji ushindi kutokana na mechi tatu zijazo ili kutawazwa wafalme wa taji la Ligue 1.

Neymar aliwaweka PSG kifua mbele katika dakika ya 33 kabla ya krosi yake nyingine kujazwa wavuni na Marquinhos dakika 26 baadaye.

Lens ambao kwa sasa wanashikilia nafasi ya tano walifutiwa machozi na Ignatius Ganago katika dakika ya 61.

Ushindi wa PSG unatazamiwa kuwapa motisha zaidi kadri wanavyojiandaa kurudiana na Manchester City ya Uingereza kwenye nusu-fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo Mei 4, 2021 ugani Etihad.

Wakicheza dhidi ya Lens, PSG walikuwa bila fowadi matata raia wa Ufaransa, Kylian Mbappe anayeuguza jeraha la mguu.

Kocha Mauricio Pochettino awaweka pia wanasoka Angel di Maria na Marco Verratti kwenye benchi japo Neymar alicheza jumla ya dakika 90 kabla ya kutolewa ugani katika dakika ya mwisho.

PSG wanaowania taji la Ligue 1 kwa msimu wan ne mfululizo, watawaendea Man-City wakilenga kubatilisha ushindi wa 2-1 uliosajiliwa na miamba hao wa Uingereza katika mkondo wa kwanza mnamo Aprili 28, 2021.

Wanasoka raia wa Uturuki, Burak Yilmaz na Zeki Celik walifunga mabao yao kutoka nje ya kijisanduku na kusaidia Lille kupiga Nice waliokamilisha mechi na wachezaji 10 pekee uwanjani. Ni pengo la alama moja pekee ndilo linawatenganisha viongozi Lille na PSG wanaoshikilia nafasi ya pili kwa pointi 75.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Chelsea waweka Fulham katika hatari ya kuteremshwa ngazi...

Real wakomoa Osasuna na kuwakaribia Atletico kileleni mwa...