• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
28,000 waliozoa ‘E’ KCSE bado wana fursa ya kufanikwa maishani

28,000 waliozoa ‘E’ KCSE bado wana fursa ya kufanikwa maishani

Na Faith Nyamai

ZAIDI ya watahiniwa 28,000 walipata alama ya ā€˜Eā€™ kwenye matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (KCSE) mwaka uliopita.Watahiniwa 141 miongoni mwao wanatoka katika shule za kitaifa.

Kulingana na Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC), wavulana wengi walipata alama hiyo ikilinganishwa na wasichana.Hili ni licha ya wavulana kufanya vyema kuliko wasichana katika matokeo ya mtihani huo.

Kwa jumla, takwimu hizo zilionyesha kuwa wanafunzi 28,046 walipata alama hiyo, ambapo 15,225 ni wavulana huku 12,821 wakiwa wasichana.

Wanafunzi 172 wenye ulemavu walipata alama hiyo kati ya wanafunzi 1,854 waliofanya mtihani.Idadi kubwa ya wanafunzi hao ilitoka katika shule za kiwango cha kaunti ndogo.

Wanafunzi hao ni 18,289.Hata hivyo, wanafunzi hao bado wana nafasi kuendelea na masomo ya kiufundi hadi katika kiwango cha uzamifu.

Wizara ya Elimu, Idara ya Mafunzo ya Kiufundi (TVET) na Mamlaka ya Kusimamia Viwango vya Kuhitimu (KNQA) zimebuni utaratibu ambapo wanafunzi wanaopata alama hiyo watapata nafasi kuendeleza masomo yao.

 

You can share this post!

Wanafunzi wengi wakosa kuripoti shuleni baada ya daraja la...

Kagwe adai shirika lilitaka kukwepa ushuru wa dawa za HIV