• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Ureno wafichua kikosi cha wanasoka 26 watakaotegemewa kuhifadhi taji la Euro

Ureno wafichua kikosi cha wanasoka 26 watakaotegemewa kuhifadhi taji la Euro

Na MASHIRIKA

MKUFUNZI Fernando Santos amefichua kikosi cha wanasoka 26 watakaotegemewa na timu ya taifa ya Ureno kwenye fainali zijazo za Euro.

Chini ya fowadi na nahodha Cristiano Ronaldo ambaye kwa sasa anachezea Juventus ya Italia, Ureno wanapigiwa upatu wa kuhifadhi taji la Euro hasa ikizingatiwa ubora wa kikosi chao kwa sasa kinachojivunia masogora wengi wa haiba kubwa.

Ronaldo ambaye ni mfungaji bora wa muda wote kambini mwa Ureno (magoli 103) ataaminiwa kuongoza safu ya mbele ya Ureno kwa ushirikiano na Bernardo Silva wa Mancheter City, Diogo Jota wa Liverpool na Joao Felix wa Atletico Madrid.

Rafa Silva wa Benfica ambaye amechezea Ureno mara 20, ametiwa pia kwenye kikosi cha kocha Fernando na atategemewa kwenye safu ya kati itakayowajumuisha wanasoka Goncalo Guedes wa Valencia na Bruno Fernandes wa Manchester United.

Ronaldo atachezeshwa pembezoni mwa uwanja huku akitarajiwa kuachia Felix na Andre Silva nafasi ya kuwa wavamizi wakuu.

Joao Moutinho na Ruben Neves wa Wolves watakuwa viungo wakabaji mbele ya William Carvalho wa Real Betis na Joao Palhinha wa Sporting Lisbon. Joao Cancelo na Ruben Dias wa Man-City watakuwa mabeki tegemeo wa Ureno huku wakitarajiwa kushirikiana na Pepe ambaye amewajibishwa na timu ya taifa mara 113.

Nuno Mendes wa Sporting na Raphael Guerreiro wa Borussia Dortmund watawania nafasi ya kuwa beki wa kushoto huku Rui Patricio, Anthony Lopes na Rui Silva wakiwania pia fursa ya kutegemewa katikati ya michuma.

KIKOSI CHA URENO:

MAKIPA: Anthony Lopes (Lyon), Rui PatrĂ­cio (Wolves) Rui Silva (Granada).

MABEKI: Joao Cancelo (Manchester City), Nelson Semedo (Wolves), Jose Fonte (Lille), Pepe (Porto), Ruben Dias (Manchester City), Nuno Mendes (Sporting CP), Raphael Guerreiro (Borussia Dortmund).

MAKIPA: Danilo Pereira (Paris Saint-Germain), Joao Palhinha (Sporting CP), Ruben Neves (Wolves), Bruno Fernandes (Manchester United), Joao Moutinho (Wolves), Renato Sanches (Lille), Sergio Oliveira (Porto) William Carvalho (Real Betis).

WAVAMIZI: Pedro Goncalves (Sporting CP), Andre Silva (Eintracht Frankfurt), Bernardo Silva (Manchester City), Cristiano Ronaldo (Juventus), Diogo Jota (Liverpool), Goncalo Guedes (Valencia), Joao Felix (Atletico Madrid) Rafa Silva (Benfica).

You can share this post!

Chelsea kutumia Abraham na Kepa kushawishi Spurs kuwapa...

Dalili kocha Ronald Koeman atapigwa kalamu na Barcelona...