• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Beki Danny Rose ajiunga na Watford baada ya kuagana na Spurs

Beki Danny Rose ajiunga na Watford baada ya kuagana na Spurs

Na MASHIRIKA

BEKI Danny Rose ametia saini mkataba wa miaka miwili na kikosi cha Watford baada ya kuagana rasmi na Tottenham Hotspur aliowachezea kwa kipindi cha miaka 14 kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Rose mwenye umri wa miaka 30 amewajibishwa na Uingereza mara 29, mara ya hivi karibuni zaidi ikiwa 2019. Nyota huyo aliwahi kuwajibikia Watford kwa mkopo wa msimu mmoja mnamo 2009.

Hakuchezeshwa na Spurs katika mchuano wowote msimu uliopita wa 2020-21 na badala yake akawajibishwa zaidi kwenye kikosi cha chipukizi wasiozidi umri wa miaka 23.

Rose alicheza katika EPL kwa mara ya mwisho mnamo Julai 2020 akiwa kambini mwa Newcastle United kwa mkopo.

Alifungia Spurs jumla ya mabao 10 katika kipindi alichohudumu kambini mwa kikosi hicho na akawa sehemu ya timu iliyoshiriki fainali ya League Cup mnamo 2015 na kuzidiwa maarifa na Chelsea kabla ya kushindwa na Liverpool kwenye fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo 2019.

Miezi saba baada ya kucheza dhidi ya Liverpool katika mechi waliyopoteza, Rose alitumwa kwa mkopo hadi Newcastle baada ya kushindwa kupata uhakika wa kuunga kikosi cha kwanza chini ya kocha Jose Mourinho.

Rose kwa sasa anajiunga na Watford waliopandishwa ngazi kushiriki EPL msimu huu baada ya kuambulia nafasi ya pili kwenye Ligi ya Daraja la Kwanza (Championship) mnamo 2020-21.

Watford watafungua kampeni zao za EPL katika msimu wa 2021-22 dhidi ya Aston Villa uwanjani Vicarage Road mnamo Agosti 14, 2021.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Kenya yapoteza fursa kuandaa mashindano ya mpira wa vikapu...

SRC yazima nyongeza ya mishahara katika sekta ya umma