• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Kenya yapoteza fursa kuandaa mashindano ya mpira wa vikapu ya wanawake ya Afrika ya Zoni ya Tano

Kenya yapoteza fursa kuandaa mashindano ya mpira wa vikapu ya wanawake ya Afrika ya Zoni ya Tano

GEOFFREY ANENE na PHILIP ONYANGO

MATUMAINI ya Kenya kuandaa mashindano ya mpira wa vikapu ya wanawake ya Afrika ya Zoni ya Tano kwa mara ya kwanza tangu 2008 yalizimwa pale ilipopokonywa uenyeji.

Mashindano hayo ya kufuzu kushiriki Kombe la Afrika (AfroBasket) baadaye mwaka huu, yamepelekwa nchini Rwanda mnamo Julai 12-17.

Shirikisho la Mpira wa Vikapu barani Afrika (Fiba Africa) lilikuwa limeomba Kenya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya zoni baada ya Misri kujiondoa kuandaa na kushiriki. Hata hivyo, shirikisho hilo lilisisitiza kuwa Kenya lazima iandae mashindano hayo katika ukumbi wa kimataifa wa Kasarani. Ukumbi wa Nyayo ni mdogo.

Katibu wa Shirikisho la Mpira wa Vikapu Kenya (KBF) Ambrose Kisoi alisema Juni 15 kuwa Kenya itaandaa mashindano hayo Julai 26-31.

Inaonekana ombi la KBF kutumia Kasarani halikufaulu kwa hivyo Kenya Lionesses sasa italazimika kusafiri hadi mjini Kigali kuwania tiketi hiyo moja.

Aidha, timu za KPA zilielekea mjini Lilongwe kwa mashindano mengine ya kimataifa ya Malawi baada ya kutesa mjini Blantyre.

  • Tags

You can share this post!

Ongwae kuhama Bears nchini Denmark baada ya kuichezea miaka...

Beki Danny Rose ajiunga na Watford baada ya kuagana na Spurs