• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:50 AM
Hafnaoui ashindia Tunisia dhahabu ya uogeleaji kwenye Olimpiki

Hafnaoui ashindia Tunisia dhahabu ya uogeleaji kwenye Olimpiki

Na MASHIRIKA

MWOGELEAJI Ahmed Hafnaoui wa Tunisia aliduwaza wapinzani wake kwa kushinda nishani ya dhahabu ya 400m freestyle kwenye Olimpiki katika ukumbi wa Aquatics Centre, Japan mnamo Jumapili.

Mpiga mbizi huyo mwenye umri wa miaka 18 aliibuka mshindi licha ya kusajili muda wa chini zaidi kwenye hatua ya mchujo. Alimpiku nambari mbili Jack McLoughlin wa Australia kwa kuandikisha muda wa dakika 3:43.36. Kieran Smith wa Amerika aliridhika na nishani ya shaba.

“Siamini kabisa. Hii ni kama ndoto iliyojibiwa. Ni fahari na tija tele kuibuka mshindi. Haya ni mashindano bora zaidi ambayo nimewahi kushiriki,” akasema Hafnaoui.

Ushindi huo ulizolea Tunisia medali ya tano ya dhahabu kwenye Olimpiki na ya tatu kutokana na mashindano ya uogeleaji.

Hafnaoui ni mwana wa mwanavikapu wa zamani wa timu ya taifa ya Tunisia, Mohamed Hafnaoui. Aliwahi kushiriki Olimpiki za Chipukizi mnamo 2018 na akaambulia nafasi ya nane kwenye 400m freestyle na nambari saba kwenye 800m freestyle.

Mnamo 2019, aliambia gazeti la La Presse nchini Tunisia kwamba maazimio yake ni kuzoa nishani ya dhahabu kwenye Olimpiki za 2024 jijini Paris, Ufaransa.

Hafnaoui ataanza kuwania medali yake ya pili ya dhahabu kwenye Olimpiki za Tokyo kwa kushiriki mchujo wa 800m freestyle mnamo Julai 26.

Yui Ohashi, 25, wa Japan naye alishinda dhahabu kwenye 400m medley baada ya kuwapiku Waamerika wawili –Emma Weyant (4:32.76) na Hali Flickinger (4:34.90).

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

KDF yaungana na GSU, Kenya Prisons na KPA fainali za...

Ongare aangushwa kwenye pigano Olimpiki