• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 4:48 PM
Ongare aangushwa kwenye pigano Olimpiki

Ongare aangushwa kwenye pigano Olimpiki

NA CHARLES ONGADI

MATUMAINI ya bondia Christine Ongare kunyanyua medali katika Michezo ya Olimpiki Tokyo Japan yaliyeyuka kama moshi baada ya kupoteza pigano lake .

Ongare alishindwa na Magno Irish kutoka Ufilipino kwa alama 5-0 katika mrindimano ulioandaliwa katika ukumbi wa Kokugikan Arena .

Majaji wote watano, Mokretarl Sidali kutoka Algeria, Muhiddinov Mansur (Tjk), Anco Bobadilla Miguel (Peru), Campbell Beau (Marekani) na Rahen Carl (Australia) walimpatia ushindi Irish katika raundi zote tatu.

Katika pigano hili, Ongare alionekana kuzidiwa maarifa na Magno aliyeonekana kumakinika na kutatiza juhudi zake .

Ongare alifuzu kuwakilisha taifa katika Michezo ya Olimpiki katika mashindano ya kufuzu ya bara la Afrika yaliyoandaliwa Dakar nchini Senegal Februari mwaka jana (2020).

Matokeo haya yamezima kabisa ndoto ya Ongare kuwa mwanamke wa kwanza nchini kushinda medali katika Michezo ya Olimpiki.

Kushindwa kwa Ongare ni pigo zaidi kwa kikosi cha taifa ‘ Hit Squad’ baada ya nahodha wake Nick ‘ Commander ‘ Okoth kupoteza pigano lake mikononi mwa Erdenebat Tsendbaatar wa Mongolia.

Matokeo haya yamewacha taifa na mabondia wawili Elizabeth ‘ Black Current ‘ Akinyi katika uzito wa welter na Elly Ajowi katika heavy.

Akinyi antarajiwa kupanda ulingoni siku ya jumanne katika jaribio lake la kulipiza kisasi dhidi ya Panguana Alcinda Helena wa Msumbiji.

Panguani amewahi kumshinda Akinyi katika mashindano ya Africa Zone 3 Championship yaliyoandaliwa DRC .

Hata hivyo, Akinyi amejiandaa barabara kumkabili Panguana katika pigano analoamini atalipiza kisasi baada ya kurekebisha makosa yaliyojiri katika pigano lao la kwanza nchini DRC.

Kwa upande wake Ajowi amesema yuko tayari kukabilinana na Cruiz Julio wa Cuba licha ya kuwa bingwa mara nne wa Mashindano ya dunia na pia ya Olimpiki katika uzito wa light heavy.

  • Tags

You can share this post!

Hafnaoui ashindia Tunisia dhahabu ya uogeleaji kwenye...

Kocha wa ndondi adai Okoth alishinda