• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 2:33 PM
Kocha wa ndondi adai Okoth alishinda

Kocha wa ndondi adai Okoth alishinda

NA CHARLES ONGADI

KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya ndondi Musa Benjamin anaamini nahodha Nick  ‘Commander’ Okoth alishinda pigano lake dhidi ya Erdenebat Tsendbaatar wa Mongoli.

Akizungumza na wanahabari baada ya uamuzi wa majaji uliompatia Tsendbaatar ushindi wa alama 3-2. Kocha Benjamin amesema uamuzi duni uliponza juhudi za Okoth kusonga mbele katika mashindano haya ya Olimpiki yanayoandaliwa katika ukumbi wa Kokugikan Arena, Tokyo nchini Japan.

“ Okoth alirusha ngumi zake vizuri na akapambana vyema akipiga more point punches ila uamuzi wa majaji ukawa ndivyo sivyo, “ akasema kocha Benjamin kwa masikitiko.

Katika pigano hili, Okoth na Tsendbaatar walionekana kuwa nguvu sawa katika raundi ya kwanza la pigano hili ila katika raundi ya Mmongolia akaonekana kulemewa na kulazimika kumshika kila mara Okoth.

Kocha Benjamin amesema kunahitajika kuwa na semina kwa majaji kuhusu namna ya kutoa alama kwa sababu washiriki wanatoka katika mataifa mbali mbali yaliyo na mitindo yao ya kutoa alama.

Hata hivyo, kocha Benjamin amesema wala hawanuii kukata rufaa kuhusu matokeo haya hasa wakizingatia sheria na masharti ya kamati ya kimataifa Olimpiki (IOC) kuhusu mashindano haya.

Aidha, kulingana na Okoth alifahamu barabara kuibuka na ushindi katika pigano hili hasa baada ya kumiliki vilivyo raundi ya pili na tatu ya pigano hili.

“ Mara baada ya kengele ya tamati nilifahamu nimeshinda pigano hili ila matokeo kutangazwa kinyume na matarajio yangu,” akasema Okoth kwa masikitiko.

Licha ya matokeo hayo, Okoth anasema anaamini ndiye mshindi wa pigano hili ambalo ndilo lake la mwisho katika michezo ya Olimpiki.

Okoth hata hivyo amewashauri wenzake wawili waliosalia kinyang’anyironi kupambana hadi mwisho baada ya kushuhudi maamuzi y a majaji.

Aliyekuwa bingwa wa taifa Keneth ‘ Valdez ‘ Okoth amempngeza OKoth kwa kupigana kijasiri katika pigano hili .

Mshidni wa medali ya shaba katika Michezo ya Olimpiki ya Los Angeles, Marekani mwaka wa 1984, Ibrahim ‘ Surf ‘ Bilali amepinga matokeo ya majaji hao akisema yalitolewa kwa mapendeleo makubwa.

Bilali: “ Okoth alishinda katika raundi ya pili na ya tatu lakini nashangazwa na uamuzi wa majaji watano waliosimamia pigano hili.”

Bondia mwingine kutoka nchini Christine Ongare amesalimu amri dhidi ya Manglo Irish wa Ufilipino kwa alama 5-0 katika pigano lililochezwa leo alfajiri .

Matokeo haya yanaiwacha Kenya na mabondia wawili pekee Elizabeth ‘ Black Current ‘ Ongare (welter) na Elly Ajowi (heavy) katika Mashindano haya ya Olimpiki .

Mabondia hawa wanatarajiwa kuingia ulingoni siku ya jumanne kupeperusha bendera ya taifa katika mashindano haya.

  • Tags

You can share this post!

Ongare aangushwa kwenye pigano Olimpiki

Sancho sasa atambulishwa kwa mashabiki