• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Natembeya awatimua maafisa wa usalama

Natembeya awatimua maafisa wa usalama

NA RICHARD MAOSI

MRATIBU wa Bonde la Ufa George Natembeya amewapiga kalamu maafisa kadhaa wa usalama kutoka Nakuru Kaskazini kwa kile alichokitaja kama utepetevu kazini.

Waliopoteza kazi ni Naibu kamishna wa Kaunti Ndogo ya Nakuru Kaskazini Bw Geoffrey Mwani Manyanna,msaidizi wa kamishna kutoka eneo la Kiamaina Isaac Ooko, Naibu Kamanda wa Polisi Benard Wamugunda na OCS wa Kituo cha Polisi Cha Kiuguini Solomon Wamae.

Aidha chifu wa kijiji cha Kabatini John Thuo na naibu wake John Mbugua walipigwa na shoka hilo , wakingana na wenzao kutoka kijiji jirani cha Thayu kuangukiwa pia kufutwa.

Natembeya alieleza kuwa hii ni baada ya uchunguzi kubaini kuwa watu nane walioaga dunia wiki iliyopita katika eneo bunge la Bahati, wakibugia pombe haramu walibugia methanol.

Akizungumza na Taifa Leo, alisema kuwa baadhi ya maafisa walikuwa wamezembea kazini licha ya kutwikwa jukumu la kuwalinda raia.

Alitumia fursa hiyo kutoa onyo kali kwa maeneo la Kilgoris, Bomet, Kajiado, Trans-Nzoia, laikipia na Marakwet, akizitaja kama sehemu sugu zinazoendeleza uuzaji wa pombe haramu.

“Kuanzia leo hatutakubali maafisa kuketi ofisini bila kuwahudumia watu kwa sababu serikali inatumia hela nyingi kuwalipa mishahara,”akasema.

Aliwaomba maafisa wa usalama kuwa macho kila wakati ili kuchunguza bidhaa ghushi zinazoingia katika soko na hatimaye kuwadhuru raia.

Aliahidi kutumia huduma za ujasusi kubaini ubora wa bidhaa, ikizingatiwa kuwa wale ambao wamepatiwa jukumu hilo ni wafisadi.

Hili linajiri siku chache baada ya Gavana wa Nakuru Lee Kinyanjui kutangaza vita, dhidi ya wauzaji pombe haramu katika mitaa ya mabanda Kaunti ya Nakuru.

You can share this post!

Polisi sita wanaohusishwa na mauaji ya ndugu wawilli wa...

Lungu akubali rungu la Hichilema nchini Zambia