• Nairobi
  • Last Updated May 24th, 2024 12:59 PM
Pasta matatani kukwamilia pikipiki aliyoazima imsaidie kuhudhuria mkutano wa injili

Pasta matatani kukwamilia pikipiki aliyoazima imsaidie kuhudhuria mkutano wa injili

NA JOHN MUSYOKI

PASTA aliyeazima pikipiki ya muumini wake kwenda kuhudhuria krusedi, alizomewa vikali alipokosa kurejesha pikipiki hiyo kwa muda aliopatiwa na kuanza kazi ya bodaboda.

Duru zinasema muumini alimpatia pasta pikipiki na kumnunulia mafuta ya Sh500.

Baada ya pasta kutoka krusedi, alikataa kurudisha pikipiki akidai alikuwa mgonjwa na pikipiki ilikuwa imepata hitilafu.

Cha kushangaza ni kwamba, pasta huyo alikuwa na mpango wa kufanya biashara ya uchukuzi mtaani ili kujipa faida kabla ya kurudisha pikipiki.

Hata hivyo, muumini alikutana naye kisadfa mtaani na kumfokea vikali kabla ya kuchukua pikipiki yake na kuondoka.

“Huna shukrani hata kidogo. Ulidanganya wewe ni mgonjwa na naona ukiwa buheri wa afya. Leta pikipiki yangu na utembee kwa miguu hadi kwako,” muumini alisema na kuondoka.

  • Tags

You can share this post!

Shirleen analenga kutamba kinoma katika uigizaji

Aliyeajiriwa kulisha mifugo ashtakiwa kwa kuuza...

T L