• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Afueni serikali ikiongezea wanafunzi muda kutuma maombi ya mkopo Helb

Afueni serikali ikiongezea wanafunzi muda kutuma maombi ya mkopo Helb

Na DAVID MUCHUNGUH

WAZIRI wa Elimu Ezekiel Machogu jana aliongeza muda wa wanafunzi kutuma maombi ili kupata ufadhili wa elimu ya juu kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Bw Machogu alichukua hatua hiyo kutokana na idadi ndogo ya wanafunzi ambao walikuwa wametuma maombi ya kupata mkopo au ufadhili wa masomo yao kwenye Vyuo vya Vikuu na pia Vyuo vya Kiufundi (TVET).

Wanafunzi hao sasa wamepewa hadi Oktoba 7 kuwasilisha maombi yao. Mwanzoni makataa hayo yalikuwa yatamatike leo lakini ni wanafunzi 156,532 pekee waliokuwa wamewasilisha maombi badala ya 265,000 waliokuwa wakitarajiwa.

Mtandao wa kuomba ufadhili huo ulifunguliwa Julai 31, 2023 na hadi jana, wanafunzi 108, 468 hawakuwa wametuma maombi.

Baadhi ya wanafunzi walikuwa wamelalamika kuwa mfumo wa kutuma maombi ulikuwa unachukua muda kabla ya kukubali maelezo yao huku wengine wakisema hawana vifaa vya kuwasilisha maombi yao mtandaoni.

“Hazina ya Fedha ya Vyuo Vikuu (UF) na Bodi ya Kutoa Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB) zimeamrishwa ziweke mikakati ya kuharakisha mchakato wa kuwapa basari na kutoa ufadhili kwa wanafunzi wote ambao wametuma maombi,” akasema Bw Machogu.

Pia Wizara ya Elimu imeondoa sharti ya kuwa lazima mwanafunzi awe na kitambulisho cha kitaifa.

  • Tags

You can share this post!

Akothee ashambuliwa kwa kuvalia nusu uchi akitumbuiza...

Nimripoti mama kwa babangu? Sababu nilimuona akichepuka na...

T L