• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:07 PM
Ajenti wa safari za ng’ambo ashtakiwa kwa ulaghai wa Sh80,000

Ajenti wa safari za ng’ambo ashtakiwa kwa ulaghai wa Sh80,000

NA RICHARD MUNGUTI

AJENTI wa kusaidia watu kutembelea mataifa ya ng’ambo ameshtakiwa kwa ulaghai wa Sh80,000.

Mark Tiapet Njenga alifikishwa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Milimani Ben Mark Ekhubi.

Tiapet alikana alimlaghai Michael Ndabi Muchege Sh80,000 akimdanganya angemsaidia kusafiri hadi nchini Amerika.

Hakimu alifahamishwa kwamba Tiapet alipokea pesa hizo kati ya Novemba 23, 2022 na Machi 8, 2023.

Ajenti huyo aliomba aachiliwe kwa dhamana akisema “nilikuwa nje kwa dhamana ya polisi ya Sh50,000.”

Baada ya kukana shtaka, hakimu alimuuliza mshtakiwa ikiwa amejaribu kumuuliza mlalamishi wasuluhishe kesi hiyo nje ya mahakama.

“Siku hizi mahakama zinapendekeza watu wakitofautiana wajaribu kupatana ili kupunguza idadi ya kesi ndogondogo kulundikana mahakamani,” Bw Ekhubi alisema.

Mshtakiwa alisema hajazungumza na mlalamishi kusuluhisha kesi hiyo.

Mshtakiwa aliachiliwa kwa dhamana ya Sh80,000 pesa taslimu.

Tiapet aliagizwa arudi tena kortini Juni 21 kesi itengewe siku ya kusikilizwa.

  • Tags

You can share this post!

Upekee wa punda wa Lamu katika uchukuzi na usafirishaji...

Okutoyi kuongoza Team Kenya kwenye mashindano ya tenisi ya...

T L