• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Aliyenaswa na silaha kujua hatima yake leo Ijumaa

Aliyenaswa na silaha kujua hatima yake leo Ijumaa

NA SIMON CIURI

MAHAKAMA ya Kahawa itatoa uamuzi leo Ijumaa kuhusu kesi iliyowasilishwa na upande wa mashtaka kutaka mfanyabiashara wa Nairobi anayezingirwa na utata azuiliwe na polisi.

Hii ni baada ya maafisa wa upelelezi waliokuwa wakiendelea na uchunguzi kupata bunduki 22 na risasi 500 katika afisi yake Jumatano.

Silaha hizo zilipatikana katika afisi ambayo mfanyabiashara huyo amekuwa akitumia eneo la Kilimani.

Hivi majuzi, landilodi wake alienda kortini ambapo alipewa amri ya mahakama kunadi bidhaa zilizomo ndani ya afisi ya Bw Okello.

Ni baada ya kuingia majengo hayo ambapo maafisa wa polisi walioandamana na madalali walipata silaha hizo hatari.

Alipowasili mbele ya Hakimu Mkuu, Bi Diana Mochache, katika Mahakama ya Kahawa, Kiambu, ambayo hujishughulisha na kesi zinazohusu ugaidi, Bw Lugwili alionekana mnyonge na dhaifu.

Mawakili wake Bw Simon Mburu na Anthony Mburu walipinga shinikizo kutoka kwa upande wa mashtaka kupitia wasilisho maalum kortini linalotaka mshukiwa azuiliwe kwa siku tano huku uchunguzi ukiendelea.

  • Tags

You can share this post!

Madaktari wanane kushtakiwa kwa kifo cha Maradona

Ruto azidi kuhusishwa na kesi ya ICC

T L