• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 7:50 AM
Asimulia alivyotapeliwa kwa jina la Ruto

Asimulia alivyotapeliwa kwa jina la Ruto

Na Richard Munguti

MKURUGENZI wa kampuni ya Makindu Motors inayouza pikipiki, alisimulia  kortini jinsi walivyoporwa tarakilishi 2,800 zenye thamani ya Sh180 milioni na watu waliojifanya kuwa wafanyakazi katika afisi ya Naibu Rais William Ruto.

Bw Charles Kamolo Musinga alimweleza hakimu mkuu mahakama ya Milimani, Nairobi, Bi Martha Mutuku walivyopelekwa katika afisi ya Dkt Ruto na mwanamke aliyejitambua kama Bi Muhoro (Joy Wangari Mukami).

Bw Musinga alisema mshukiwa huyo alishirikiana na wengine, ambao ni Allan Kiprotich Chesano, Teddy Awiti, Kelvin Matundura Nyongesa, James William Makokha almaarufu Mr Wanyonyi na Joram Ochieng Osore.

Alisema Bi Muhoro alikutana nao katika hoteli ya Java, Karen na Ole Seren ambapo walielezwa watoe fedha Sh500,000 za kufanikisha kupewa kandarasi hiyo ya kuuzia afisi ya Dkt Ruto tarakilishi hizo.

Bw Musinga alisema walipeleka tarakilishi hizo zote katika wizara ya fedha mtaani Eastleigh Nairobi lakini hawakulipwa pesa hizo.

  • Tags

You can share this post!

Mbunge akamatwa kuhusu mapigano Kapedo

Wapinzani taabani Ruto akiidhinishwa kuongoza Wakalenjin