• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
Awamu ya tatu ya Kazi Mtaani yazinduliwa nchini

Awamu ya tatu ya Kazi Mtaani yazinduliwa nchini

NA WINNIE ONYANDO

AWAMU ya tatu ya mpango wa Kazi Mtaani unaolenga kutoa ajira kwa vijana zaidi ya 900 wanaotoka katika mitaa ya mabanda umezinduliwa rasmi katika kaunti mbalimbali.

Usajili wa vijana katika mpango huo ulizinduliwa mnamo Novemba 19, 2021.

Kamisha wa Kaunti ya Bomet, Susan Waweru aliongoza hafla ya uzinduzi huo huku akisema utasaidia pakubwa vijana wanaotoka katika kaunti hiyo wasio na kazi.

Kwa upande mwingine, kamishna wa eneo la Bonde la Ufa, Mohammed Maalim alisimamia uzinduzi huo wa awamu ya tatu ya mpango wa Kazi Mtaani katika Kaunti ya Samburu.

Awamu hiyo ya tatu ya mpango wa Kazi Mtaani pia ilizinduliwa katika Kaunti za Kisumu, Nyandarua na Kilifi.

Wakati wa uzinduzi wa usajili, Katibu Mkuu anayesimamia mpango wa Kazi Mtaani, Charles Hinga alisema kuwa awamu hiyo ya tatu itakuwa thabiti na bila ubaguzi.

“Tunafahamu kuwa vijana wengi walitegemea mpango huu wa Kazi Mtaani. Tunafurahi kuurejesha kwa kuwa zaidi ya vijana 900 kutoka kila kaunti nchini watapata ajira,” alisema Bw Hinga.

  • Tags

You can share this post!

ZARAA: Jinsi ushirikiano kati ya serikali na sekta ya...

Kang’ata apuuza madai kuhusu kuzimwa kwake

T L