• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 2:24 PM
Bei ya mafuta yabaki pale pale

Bei ya mafuta yabaki pale pale

NA CHARLES WASONGA

NI afueni kidogo kwa wenye magari na Wakenya kwa ujumla baada ya serikali kudumisha bei ya sasa ya mafuta kwa kipindi cha kati ya Aprili 15, 2023 hadi Mei 14, 2023.

Kulingana na tangazo lililotolewa na Mamlaka ya Kusimamia Kawi na Mafuta Nchini (EPRA) bei ya mafuta aina za petroli, dizeli na mafuta taa zitasalia Sh179.30, Sh162 na Sh145.95 kwa lita moja, mtawalia, jijini Nairobi na viunga vyake.

“Katika kipindi kijacho, bei za rejareja za mafuta aina ya petroli, dizeli na mafuta taa hazitabadilika,” EPRA ikasema kwenye taarifa Ijumaa Aprili 14, 2023.

Hii ni kwa sababu serikali imetoa ruzuku kwa bei za dizeli na petroli ilhali ruzuku ya Sh17.12 kwa lita imedumishwa kwa mafuta taa.

Serikali itatumia pesa zinazokusanywa kupitia ushuru wa ustawi wa petroli kuzifidia kampuni za kuuza mafuta kwa kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya chini.

Serikali imedumisha bei ya mafuta licha ya kupanda kwa bei ya petroli inayoagizwa kutoka nje.

Kwa mfano, bei ya bidhaa hiyo imepanda kwa kima cha asilimia 1.07 kutoka dola 659.47 (Sh91,670) wa pipa mwezi Februari hadi dola 666.51  (Sh92.643) kwa pipa mwezi wa Machi, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Mbunge aitaka kampuni ya Kenyatta kumlipa Sh10 milioni

Gachagua: Transfoma za wanaume Mlima Kenya zimezima kwa...

T L