• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
Cherargei ambebesha lawama waziri Namwamba kwa mkanyagano Kericho

Cherargei ambebesha lawama waziri Namwamba kwa mkanyagano Kericho

NA LABAAN SHABAAN

SENETA wa Nandi Samson Cherargei amemlaumu Waziri wa Michezo Ababu Namwamba kwa mkanyagano uliosababisha vifo vya watu watano  kwenye hafla ya kitaifa ya Mashujaa Dei, Ijumaa, katika Kaunti ya Kericho.

Polisi na wauguzi walithibitisha kuwa watu wengine 13 waliponea na wakatibiwa.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, Seneta Cherargei alitaja tukio hilo kuwa la aibu na kumtaka Waziri Namwamba kuwajibika.

“Wizara ya Michezo ya Waziri Ababu (Namwamba) inafaa kuwajibika kwa  mkasa uliotokea kwa sababu ni dhihirisho wazi kwamba maafisa wa  ukaguzi walifanya kazi duni,” akasema, huku akisisitiza ni aibu kwa taifa.

Kulingana na ripoti ya polisi, mkanyagano huo ulisababishwa na chai iliyomwagika majira ya alfajiri.

Idara ya usalama inasema, chai ya mama mchuuzi langoni mwa uga ilimwagika kwenye moto na kusababisha moshi uliodhaniwa kuwa gesi ya kutoa machozi.

Wakati watu wakitorokea usalama wao, ndipo mkanyagano huo ulipotokea.

Rais William Ruto alituma risala za rambirambi kwa waliopoteza wapendwa wao. Ingawa hivyo, baadhi ya Wakenya walilalamika kwamba alichelewa kurejelea tukio hilo.

  • Tags

You can share this post!

JAGINA: ‘Oduwo Cobra’ aliyevuma kriketi

Infantino anguruma kwa Kiswahili akizindua Ligi ya Kandanda...

T L