• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
Infantino anguruma kwa Kiswahili akizindua Ligi ya Kandanda ya Afrika almaarufu AFL

Infantino anguruma kwa Kiswahili akizindua Ligi ya Kandanda ya Afrika almaarufu AFL

NA LABAAN SHABAAN

RAIS wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela alisema ukizungumza na mtu kwa lugha anayofahamu, unachomuambia huingia kichwani mwake na ukisema naye kwa lugha yake, usemacho huingia moyoni mwake.

Msemo huu wa nguvu kutoka kwa mtu mashuhuri aliyependwa na wengi, umetumiwa kuvutia hadhira kwa hotuba.

Rais wa Shirikisho la Kandanda Duniani (FIFA) Gianni Infantino alielewa hili fika na kuutumia kuhakikisha maneno yake yanawafurahisha mashabiki wa kandanda waliofika uwanjani Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Alipopanda jukwaani kutambulisha klabu ya soka ya Simba, Infantino alizungumza kwa Kiswahili na kufurahisha maelfu ya mashabiki waliojaa ugani.

 “Simba nguvu moja! Simba nguvu moja!” Infantino alisema huku mashabiki wakisherehekea wakiinua mabango ya Simba.

 “Karibu Tanzania.. hii ni shauku, huu ni upendo, hii ni Tanzania, hii ni Afrika, hii ni Simba, hii ni Al Ahly, hii ni CAF, hii ni FIFA na hii ni kandanda. Kandanda huunganisha dunia na leo imeunganisha dunia kutoka Tanzania,” aliongeza.

Rais wa FIFA alihutubu Ijumaa, Oktoba 20, 2023, alipokuwa anazindua Ligi ya Kandanda ya Afrika (AFL).

Alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri wa kimataifa waliohudhuria hafla iliyopisha ligi mpya.

Mashindano haya yanatarajiwa kuimarisha kandanda ya klabu barani.

Simba SC ya Tanzania na Al Ahly ya Misri zilishiriki mechi ya ufunguzi na kupata sare ya 2-2.

  • Tags

You can share this post!

Cherargei ambebesha lawama waziri Namwamba kwa mkanyagano...

Pasta aweka Biblia kando na kumlima polo aliyemtorosha mkewe

T L