• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:55 AM
Chifu ashambuliwa kwa kujaribu kusimamisha disko matanga Kisumu

Chifu ashambuliwa kwa kujaribu kusimamisha disko matanga Kisumu

NA MERCY KOSKEI

CHIFU  mmoja kutoka Kaunti ya Kisumu anauguza majeraha baada ya kushambuliwa na wanakijiji wenye ghadhabu, alipokuwa akijaribu kusimamisha muziki wakati wa ‘disco matanga’.

Kisa hicho kilitokea wikendi katika kijiji cha Nduru Kaunti ndogo ya Kadibo.

Chifu huyo wa lokesheni ya Kawino Kusini kwa jina Michael Buodo alifika eneo hilo Jumamosi usiku Septemba 16,2023 kuwazuia kucheza muziki kwa sauti ya juu kwenye mkesha huo.

Jaribio lake la kuwafukuza liliwakera vijana hao ambao waligeuza ghadhabu yao kwake, na kumshambulia kwa panga na kumuacha na majeraha mgongoni, kichwani, na mguu wake wa kulia.

Bw Buodo alikimbizwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOTRH) na wasamaria wema ambapo alitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Akizungumza na stesheni moja Jumanne asubuhi Septemba 19,2023,  Chifu huyo alidokeza kuwa bado ana maumivu mwilini.

Bw Buodo alifichua kuwa  aliwatambua vyema vijana hao wakorofi waliomshambulia licha ya shambulizi kutokea usiku.

Kulingana na Naibu Kamishna wa Kaunti ndogo ya Kadibo, Bw George Onyango, suala hilo linachunguzwa na kuhakikisha kuwa waliohusika na shambulizi hilo watakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

  • Tags

You can share this post!

Al-Shabaab: Wakazi wafanya maandamano kuitaka serikali...

Hasla: Wachuuzi 40 wazuiwa kufanya biashara zao mjini

T L