• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 6:55 PM
DCI yaonya wasichana dhidi ya walaghai mtandaoni

DCI yaonya wasichana dhidi ya walaghai mtandaoni

Na MARY WANGARI

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) imetoa ilani kuhusu matapeli wanaowavizia wasichana mitandaoni kwa kutumia ahadi za uongo na kisha kuwalaghai pesa zao.

Kulingana na taarifa kutoka kwa DCI, matapeli hao hujitokeza kama wafanyabiashara tajiri huku mitandao yao ya kijamii ikiwa imejazwa picha zinazoonyesha maisha yao ya kifahari.

Matapeli hao ambao upelelezi umeonyesha wanatoka Kisumu na Kiambu, huwashawishi wasichana kwa kuwaahidi maisha ya kifahari Ulaya na kuwavutia kwa zawadi ghali kama ishara ya mapenzi yao ya dhati.

“DCI inawatahadharisha wanawake chipukizi mitandaoni kujihadhari na matapeli wanaowahadaa kwa ahadi za kuwapa maisha mazuri Ulaya, lakini wanaishia kuwapunja pesa zao.”

“Hii ni baada ya maafisa wenzetu katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jommo Kenyatta (JKIA) kuingiwa na wasiwasi kutokana na kuongezeka kwa wasichana wanaofurika katika uwanja huo kwa madai ya kuchukua zawadi walizotumiwa na “wapenzi” wao waliopatana kupitia mitandao ya kijamii.”

“Wanapofika, huwa wanashtuka kutambua walitapeliwa na hakuna zawadi zozote zilizotumwa,” ilisema taarifa kutoka kwa DCIKatika kisa cha hivi punde, mwanamke mwenye umri wa miaka 28 alitapeliwa Sh52,000 baada ya kukutana na mwanamume kwenye mitandao ya kijamii aliyedai kuwa raia wa Uingereza.

Kama ishara ya mapenzi yake, tapeli huyo alidai alimtumia mwanamke huyo mikufu na mapambo mengine ya dhahabu.Kabla ya kupokea zawadi hizo alipokea simu kutoka kwa mwanamume aliyejitambulisha kama afisa wa kukusanya ushuru wa bidhaa zinazoingizwa nchini katika JKIA, aliyemjulisha kuwa amepokea kifurushi chake kutoka Ulaya, na kwamba alihitajika kulipa ada ya Sh52,000 ili kukichukua.

“Alipowasili JKIA, simu ya mwanamume aliyejifanya kuwa ajenti wa kupitisha bidhaa haikuchukuliwa,”“Uchunguzi umeonyesha kuwa wakora hao huendesha shughuli zao kutoka Kisumu na Kiambu,” ilisema DCI.

You can share this post!

Wagonjwa 18 wa corona wafa moto ulipozuka kwenye wodi

Hatua ya Waiguru kutimua madaktari yamtatiza