• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:55 AM
DPP kumshtaki afisa wa polisi kwa mauaji ya bucha Kiamaiko

DPP kumshtaki afisa wa polisi kwa mauaji ya bucha Kiamaiko

Na RICHARD MUNGUTI

MKURUGENZI wa Mashtaka ya Umma (DPP) ameagizwa amshtaki kwa mauaji afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua bucha aliyekuwa akichinja mbuzi katika soko la Kiamaiko mtaani Huruma kaunti ya Nairobi miaka sita iliyopita.

Hakimu mkuu mahakama ya Milimani Bw Francis Andayi aliamuru afisa wa polisi David Kibet Rono akamatwe na kushtakiwa kwa mauaji ya Nura Malicha.Nura, aliyekuwa na umri wa miaka 20 aliuawa mnamo Aprili 20,2015 Kiamaiko kwa madai alikuwa amemwibia Jessie Njeri simu aina ya Techno.

Lakini hakimu alisema Bw Rono na afisa mwingine wa polisi Bw Ali Bakari waliokuwa wakishika doria walijikanganya katika ushahidi wote kortini.Wawili hao walisema Nura alijaribu kumndunga kisu Rono ndipo akampiga risasi kwenye shavu na tumboni.

“Meno matatu ya Nura yalitoka alipotwangwa risasi ya shavu,”alisema Bw Andayi.Hakimu aliongeza kusema mhasiriwa huyo pia alipigwa risasi tumboni.Akitoa uamuzi katika uchunguzi wa kubaini kilichosababisha kifo cha Nura, Bw Andayi alisema mshtakiwa aliuawa na Rono.

Ripoti ya Dkt Carolyne Njeru, aliyefanyia uchunguzi maiti ya Nura ilisema risasi tatu zilitolewa katika mwili wa mhasiriwa huyo.Hakimu alisema ushahidi uliowasilishwa na mamlaka huru ya polisi (IPOA) umethibitisha Nura aliuawa na Rono.

Hakimu mkuu wa Nairobi Francis Andayi…Picha/RICHARD MUNGUTI

“Baada ya kutilia maanani ushahidi wote nimefikia uamuzi Nura aliuawa na afisa wa Polisi Bw Rono,” alisema Bw Andayi.Hakimu alisema lazima haki itendeke kwa kufunguliwa mashtaka dhidi ya Rono kwa mauaji ya Nura.

Bw Andayi aliamuru uamuzi wake uwasilishwe kwa DPP Bw Haji amfungulie mashtaka Bw Rono.Hakimu alisema mashahidi 14 walitoa ushahidi katika uchunguzi huo.

  • Tags

You can share this post!

Washirika wa vigogo wasisitiza mwaniaji wao ndiye astahili

Hofu idadi ya maambukizi ya corona ikipanda tena nchini