• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
Eneo Kiambu ambapo vijana hawavuti bangi, kunywa pombe wala kushiriki ukahaba

Eneo Kiambu ambapo vijana hawavuti bangi, kunywa pombe wala kushiriki ukahaba

NA RICHARD MAOSI

JE, unajua katika Kenya hii yetu mji wa Kijabe unaopatikana Kaunti ya Kiambu hakuna baa, makahaba, vilabu wala uvutaji sigara?

Baadhi ya wafanyibiashara wamekiri kwamba wamewahi kuanzisha biashara za kuuza pombe, lakini hazikufika mbali kwa sababu walikosa wateja.

Aidha, vyumba vya kulala hapa maarufu kama lojing’i hukodishwa na wachumba ambao wamefunga ndoa, na mara nyingi huwa wamebeba stakabadhi kuonyesha wako ndani ya ndoa au ndoa yao ni halali.

Ni sehemu ambayo ukifungua biashara ya kuuza vileo hautapata mteja hata mmoja, kwa sababu vijana wanafuata mwongozo mzuri wa kidini.

Pili, ukizuru sehemu nyingi za Kijabe utagundua kuwa vijana hawana muda wa kuzurura na badala yake wanajishughulisha kuchapa kazi ima kwenda shambani au kuendesha boda almuradi mkono uende kinywani.

Alfred Mwangi mwendeshaji boda mjini Kijabe anasema katika kila sehemu eneo hilo lazima utakutana na kanisa.

Kulingana na Mwangi, huu (2023) ni mwake wake wa 13 kama mkazi wa Kijabe na kila anapotaka kukata stimu labda atembelee miji jirani ya Kinungi au Fly Over.

“Inashangaza ukitaka starehe, utalazimika kutembelea maeneo Jirani,” akaambia Taifa Leo Dijitali.

Anasema, hata kuvuta sigara lazima mnunuzi atafute, ajipange mapema kunua pakiti kadhaa kwa sababu maduka hapa hayana bidhaa hiyo.

Anasema wanaosimamia shughuli za usafiri pia wana uhuru wa kuingilia kati endapo watagundua madereva au makanga wanakunywa pombe au kuvuta sigara.

Kinyume na maeneo mengine ya Mkoa wa Kati kama vile Muranga, Nyeri na Kirinyaga ni dhahiri kuwa Kijabe ni kielelezo cha kuigwa miongoni mwa maeneo ambayo vijana wamezama kwenye lindi la unywaji pombe na kutumia mihadarati.

“Tunaamini kulea jamii kwa msingi wa Kikristu na maadili mema,” akasema Mhubiri John Ndirangu.

  • Tags

You can share this post!

Ajabu mwanamume kupatikana akifukua kaburi la mkewe Nakuru

Pasta Ng’ang’a afukuza walio na Digrii kanisa lake

T L