• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Faini ya Sh850,000 kwa kufichua hali ya HIV ya mwenzake katika WhatsApp

Faini ya Sh850,000 kwa kufichua hali ya HIV ya mwenzake katika WhatsApp

NA PHILIP MUYANGA

Jopo la mahakama linaloshughulikia kesi kuhusu virusi vya ukimwi (HIV and Aids Tribunal) limeamuamuru mwanamme mmoja kulipa Sh850,000 kwa kutangaza hali ya HIV ya mtu mwingine kupitia maoni yake kwa mtandao wa WhatsApp na kufanya unyanyapaa.

Pia jopo hilo limetoa agizo la kumzuia Bw FO, kama alivyotambulika katika stakabadhi za kesi, kusema hali ya HIV ya Bw PMM, kumbagua, kumfanyia unyanyapaa na kumyanyasa.

Mahakama hiyo ilisema kuwa vitendo vya FO vilikiuka sheria ya HIV na Aids Prevention and Control Act (HAPCA) na kwamba kinyume cha sheria na bila ruhusa, alisema hali ya HIV ya Bw PMM, iwapo ni kweli au ni kudhania, kwa watu wengine ambao ni wanachama wa grupu hiyo ya WhatsApp.

Jopo hilo ikiongozwa na mwenyekiti Carolyne Mboku lilibainisha kuwa ushahidi wa Bw PMM kuhusu madai ya hali ya HIV yalimfikia mke wake ambaye alitoroka katika kitanda cha ndoa na kuanza kulala katika chumba tofauti na kwamba watu katika kanisa lake waliepuka kuketi karibu naye.

“Tukichukulia ushahidi wa mlalamishi na ule uliotolewa kuunga mkono madai yake, tunapata ya kuwa mlalamishi alibaguliwa na kupitia unyanyapaa,”jopo hilo lilisema.

Jopo hilo ambalo wanachama wake wengine ni Prof WG Jaoko, NW Osiemo, BO Yogo, JN Ngoiri na Dkt S Musani pia liliagiza Bw FO kumlipa fidia ya Sh3,000 Bw PMM kama gharama ya ushauri nasaha.

Bw PMM alisema kuwa pamoja na Bw FO walikuwa katika grupu moja ya WhatsApp (la wanachama wa chama kimoja cha kisiasa eneo la Magharibi).

Alisema kuwa mnamo Julai 3 mwaka jana, walianza kuzungumza masuala ya siasa katika mtandao huo wakati aliweka maoni yake yaliyokinzana na maoni ya Bw FO kuhusiana na atakayeshinda kiti cha ubunge katika eneo bunge moja.

Bw PMM alisema kuwa mshtakiwa aliweka maoni kwa mtandao huo wa WhatsApp akidai kuwa (PMM) alikuwa na virusi vya HIV na kwamba maoni hayo yalitolewa mbele ya wanachama katika grupu hiyo na kwamba imefanya kupata unyanyapaa na kupoteza heshima.

Kulingana na PMM, aliamua kumtumia mshtakiwa ujumbe akimsihi awache kumtukana na kuweka madai ya uongo kuhusu hali yake ya HIV kwa grupu zingine za kisiasa lakini Bw FO alikuwa haonyeshi msamaha wowote kwa vitendo vyake.

Bw PMM anasema kuwa alikumbana na ubaguzi katika grupu hiyo na na grupu zingine ambapo baadhi ya watu walimkejeli na kuanza kuongea kuhusu hali yake.

Aliliambia jopo hilo kuwa alijihisi kukataliwa na wenzake kufikia kiwango cha kutokuwa na uhuru wa kueleza maoni yake kwa mitandao ya kijamii ambapo yuko.

Bw PMM alisema kuwa amepata changamoto nyingi kuanzia kijamii na kisaikolojia, na kwa sababu ya maoni ya mshtakiwa na kwamba kwa sasa anaendelea kupata ushauri nasaha.

Licha ya kupewa nafasi ya kujibu madai katika kesi hiyo, mshtakiwa hakufika mbele ya jopo na kesi iliendelea bila uwepo wake.

  • Tags

You can share this post!

Maombi mabaya ya Karen Nyamu dhidi ya Man U yaonekana...

Waliowekeza karibu na kwa Pasta Ezekiel wakadiria hasara

T L