• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 2:24 PM
Gachagua: Pombe Mlima Kenya imegeuza wanaume kuwa goigoi

Gachagua: Pombe Mlima Kenya imegeuza wanaume kuwa goigoi

NA ALEX KALAMA

NAIBU Rais Rigathi Gachagua ameachilia kombora la utani kwa wanaume wa eneo la Kati, akidai wameshindwa na majukumu muhimu ya ndoa kwa sababu ya kutekwa na ulevi.

“Naiibika kila siku nikikutana na wamama ile maneno wananiambia nashindwa na lakusema,wananiambia naibu tulikuchagua wewe na William Ruto watoto wetu wanamalizwa na pombe na mumenyamaza. Inanipa changamoto mimi kama kiongozi wa nchi hii na wa eneo hili nikiangalia kile kinachofanyika,naongea kama mzazi naongea na kina mama naongea na kina mama wachanga vijana wetu wameisha,” akasema.

Akizungumza katika eneo la Mlima Kenya Gachagua amesema inasikitisha kusikia kwamba kina baba ambao wanapaswa kulala pamoja na kina mama juu ya kitanda kuwa wao hulala chini na badala yake kuacha kina mama kulala peke yao kitandani.

“Ukienda katika shule zetu zote madarasa hayana watu, hata hii magavana ni shida mkiweka pesa kwa hizi shule ni bure maana hakuna wanafunzi. Kwa sababu ethanol inakuja ikiwa imechanganywa imemaliza kila kitu, kwa hii vijana wetu mawe iki chini na hata ikiwekwa moto bado haiwezi kufanya. Kwa hiyo kina mama zetu wanalia na huo ndio ukweli,” akasema.

Kulingana na Gachagua ni kwamba huwa watu hawapendi kusema ukweli ila vile alivyosema ndio hali halisi ilivyo eneo hilo la Mlima Kenya.

“Sisi kama viongozi tuliochaguliwa madam Waiguru gavana Kahiga Wamatangi tutafanyaje na watu wetu,tuko wapi tutawambia nini watu waliotuchagua wakati tukikutana na wao tutawaambia nini. Wakati watoto wetu wanamalizwa na ulevi na mihadarati tuko wapi tutakuwa hatuna la kuongea? Ndindi Nyoro, Kimani Ichungwa, Mathenge mtaambia watu nini? aliuliza tafadhalini hii hafla ya leo tufungue nyoyo zetu na tuweke mambo wazi.

  • Tags

You can share this post!

Gachagua: Transfoma za wanaume Mlima Kenya zimezima kwa...

Ruto azongwa na changamoto tele

T L