• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:50 AM
Gaucho afichua aliitunuka familia ya Raila nakala tatu za Biblia iliyoandikwa kwa Kiswahili

Gaucho afichua aliitunuka familia ya Raila nakala tatu za Biblia iliyoandikwa kwa Kiswahili

NA WINNIE ONYANDO

RAIS wa Bunge la Mwananchi Calvine Okoth almaarufu ‘Gaucho’ amefichua kwamba amewahi kuipelekea familia ya Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga zawadi maalum.

Akizungumza na Taifa Leo, mwanasiasa na mwanaharakati huyo alisema alipata fursa ya kuwasilisha zawadi hizo baada ya Mama Ida Odinga kumwalika nyumbani kwake Karen.

Hii, kulingana na Gaucho, ilikuwa mara tu baada ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Kenya 2017.

Japo alikutana na familia ya Bw Odinga kupitia binti yake Rosemary Odinga, Gaucho anasema kuwa alishindwa ni zawadi gani angeipa familia ya Bw Odinga.

“Baada ya Uhuru Kenyatta kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Kenya katika Uchaguzi Mkuu wa 2017, kulitokea vurugu za baada ya uchaguzi. Hata hivyo, kulikuwa na maombi maalum katika bustani ya Uhuru Park yaliyoandaliwa na David Owuor. Raila na Mama Ida pia walihudhuria mkutano huo wa maombi. Kisha mmoja wa marafiki wa familia yao aliniona na kuniita. Bi Ida aliposikia jina langu, aliniita na kuuliza ikiwa ninamfahamu bintiye Rosemary,” Gaucho akaambia Taifa Leo.

Kulingana na Gaucho, Mama Ida alimwambia kuwa binti yake Rosemary “alikuwa akinitaja kila mara.”

Alipoalikwa kutembelea familia ya Bw Odinga, hakufikiria mara mbili.

“Nilifikiria kile ningeitunuka familia ya Odinga lakini nikashindwa. Hii ni kwa sababu wanaweza kumudu chochote wanachotaka, kuanzia kwa samaki, kusafiri kwa kutumia chopa au helikopta… ikiwa ni mboga wanaweza kuinunua bila shida yoyote… Baada ya kuwaza kwa muda, niliamua kununua nakala tatu za Biblia iliyoandikwa kwa Kiswahili ambazo nilizifunga vizuri. Niliwasilisha zawadi hiyo kwa familia hiyo,” akasema Gaucho.

  • Tags

You can share this post!

Sabina Chege ajeruhiwa katika fujo zilizozuka Bungeni mnamo...

Amadi apata afueni mahakama ikiagiza akaunti zake za benki...

T L