• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Hofu fisi wakizurura vijijini

Hofu fisi wakizurura vijijini

NA GEORGE ODIWUOR

Vikundi vya fisi wamevamia baadhi ya vijiji vya Mbita kaunti ya Homa Bay na kuua mifugo na kusababisha taharuki kwa wakazi.

Wakazi wa eneo la Lambwe Mashariki waliripoti kukutana na fisi katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Baadhi ya wakulima waliripoti kupoteza mifugo yao baada ya kushambuliwa na kuuawa na wanyama hao wa porini.

Chifu wa eneo la Lambwe Mashariki Bernard Ouma alisema alipata ripoti za wakulima kupoteza punda wanane na kondoo wanne.

Alisema fisi hao hutembea kwa makundi huku wakitafuta chakula na maji. Hii imezua hofu kwa wakazi ambao sasa wanahofia kwamba wanaweza kushambuliwa pia. Vijiji vilivyoathiriwa vimezungukwa na vilima na misitu ikiwa ni pamoja na Ruri na Kibanga.

Wakazi walitoa wito kwa Shirika la Huduma ya Wanyamapori (KWS) kuwafuga wanyama hao. Afisa wa KWS katika kaunti hiyo Ziporah Mideva alisema hajapokea rasmi ripoti kuhusu wanyama hao lakini shirika litahakikisha vijiji viko salama.

“Nimesikia habari tu kupitia vyombo vya habari,” alisema.

  • Tags

You can share this post!

Jinsi walinzi wa Mshauri wa Masuala ya Usalama wa Serikali...

DONDOO: Mganga afunga kazi kwa kukosa wateja

T L