• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
IG aunda kikosi kuchunguza mauaji ya wanne

IG aunda kikosi kuchunguza mauaji ya wanne

Na NICHOLAS KOMU

KUNDI maalumu la wapelelezi lililoundwa kuchunguza kutoweka kwa wanaume wanne marafiki na hatimaye kuuawa kwa wawili kati yao limepewa mwezi mmoja kuwasilisha ripoti kwa Inspekta Jenerali wa polisi, Hillary Mutyambai.

Jana, kinara huyo wa polisi alisema ameagiza kuundwa kwa kikosi cha watalaamu wa kuchunguza mauaji kutoka Idara ya Uchunguzi wa Uhalifu, kuchunguza vifo vya wanaume watatu ambao mili yao ilipatikana Alhamisi.

Akizungumza katika chuo cha kitaifa cha mafunzo ya maafisa wa polisi cha Kiganjo, kaunti ya Nyeri, Bw Mutyambai alisema maafisa hao tayari wameanza kazi katika juhudi za kubaini wanne hao walivyotoweka na baadhi yao kuuawa.

“Kundi hilo tayari limeanza uchunguzi na linafaa kunikabidhi ripoti ndani ya mwezi mmoja,” akasema Bw Mutyambai.

Mili ya wanaume watatu ilipatikana Mathioya, kaunti ya Murang’a, Thika, na kaunti ya Kiambu siku kumi na moja baada ya marafiki hao wanne kutoweka baada ya kupata chakula cha mchana katika mkahawa mmoja mjini Kitengela.

Mili ya Elijah Obuong’, 35 na Benjamin Imbai, 30 ilitambuliwa na jamaa zao Alhamisi. Mwili wa tatu unaoshukiwa kuwa wa Jack Ochieng’, 37 ulipatikana Alhamisi Mathioya, hatua chache kutoka pale wa Obuong ulipatikana.

Jana, familia ya Jack Ochieng ilisema mwili wa tatu haukuwa wake na ungali kutambuliwa. Brian Oduor, 36, bado hajapatikana. Kufikia sasa, haijabainika kilichowapata wanaume hao ambao maisha yao yamepigwa darubini kwa kuhusishwa na uhalifu.

  • Tags

You can share this post!

Shule za kibinafsi zalalamikia ubaguzi

Miaka 10 tangu auawe na Amerika, Osama bado ana ufuasi...