• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:50 AM
Kamishna wa Kaunti ya Nakuru aagizwa kufika Kortini

Kamishna wa Kaunti ya Nakuru aagizwa kufika Kortini

Na RICHARD MUNGUTI

KAMISHNA wa kaunti ya Nakuru Bw Erastus Mbui ameagizwa afike kortini kujitetea asisukumwe jela kwa kukaidi agizo la mahakama amtunze mmiliki wa shamba la mamilioni ya pesa iliyoko Mau-Narok.

Bw Mbui anadaiwa alikaidi agizo la kuagiza polisi waanadamane msimamizi wa mali ya aliyekuwa waziri Mbiyu Koinange kuingia katika shamba la Muthera.Shamba hilo la ekari 4,290 lililoko eneo la Mau Narok.

Mahakama ya Nakuru Ijumaa ilitoa agizo Bw Mbui afike mbele yake kujitetea asifungwe kwa kudharau maagizo yake.Inadaiwa kamishna huyo wa kaunti aliagizwa Agosti 5, 2021 ahakikishe polisi wameandamana na Bw

David Njunu Koinange akielekea shambani hilo.Mahakama ilimwagiza Bw Mbui pamoja na afisa msimamizi wa polisi eneo hilo wahakikishe Bw Njunu yuko salama anapoenda shambani.Hata hivyo Bw Njunu kupitia kwa wakili Joseph Karanja Mbugua aliwasilisha kesi akiomba kamishna huyo atiwe nguvuni na kusukumwa jela kwa kukaidi agizo la kutoa usalama kwa Bw Njuni.

Hakimu mkazi wa Nakuru Bw Isaac Orenge aliyesikiza ombi la Bw Mbugua alimwamuru Bw Mbui kufika kortini Agosti 18 kujitetea na maagizo zaidi kutolewa.Katika uamuzi wake Bw Orenge alisema mlalamishi Bw Njunu amethibitisha agizo la korti halikutekelezwa na kumwagiza Bw Mbui afike kortini kutoa maelezo.

“Unatakiwa kufika kortini kueleza sababu ya kutotekeleza agizo la hii mahakama,” Bw Orenge alimwagiza Bw Mbui.Bw Njunu alieleza mahakama aliteuliwa na mahakama kuu kusimamia shamba hilo ambalo limekumbwa na mzozo mkali kati ya kikundi cha Wamaasai na  familia ya marehemu Koinange.

Mzozo huo ulipamba moto na mmamo Desemba 2010 mwanaharakati Moses ole Mpoe aliuawa pamoja na wanaume waliokuwa wanaendesha piki piki katika makutano ya barabara ya Nakuru-Eldoret-Njoro mnamo Desemba 3 2010.

  • Tags

You can share this post!

Vifaranga wapya wa Raila

Mwashetani aachia Achani tikiti ya ugavana