• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 8:50 PM
Kampuni iliyomshtaki Amadi kuhusu sakata ya dhahabu yahofia kesi inavurugwa

Kampuni iliyomshtaki Amadi kuhusu sakata ya dhahabu yahofia kesi inavurugwa

Na RICHARD MUNGUTI

KAMPUNI ya Dubai iliyomshtaki Msajili wa Mahakama Anne Amadi kwa dai la ulaghai wa Sh91.4 milioni imedai kuna njama za kuvuruga kesi hiyo katika Mahakama Kuu.

Bruton Gold Trading LLC iliyokata rufaa kupinga agizo la kufunguliwa kwa akaunti za Anne Amadi, mwanawe Brian, Andrew Njenga Kiarie na Daniel Ndegwa Kangara almaarufu Daniel Muriithi imedai Bi Amadi pamoja na Jaji mmoja wameshirikiana kuhujumu haki.

Bruton Gold Trading LLC imeeleza katika rufaa iliyowasilishwa Agosti 29, 2023 kwamba kesi iliyoshtaki katika Mahakama Kuu imeingiliwa kabisa na maagizo ya kufunguliwa kwa akaunti za Bi Amadi kulikuwa kinyume cha sheria.

Jaji Ngenye Macharia wa Mahakama ya Rufaa aliratibisha rufaa ya Bruton kuwa ya dharura.

Akaunti hizo zilizimwa polisi wakidai zilitumiwa kupokea pesa ambazo kampuni inadai ililaghaiwa katika kashfa ya dhahabu kabla ya Mahakama Kuu kuondoa kibali za kuzizima.

Kampuni hiyo inasema kwamba uchunguzi wa polisi ulionyesha kwamba Bi Amadi alipokea pesa inazodai ilitapeliwa na inaomba Mahakama ya Rufaa kutoa agizo la kuzizima tena akaunti hizo za benki.

Korti ya rufaa iliidhinisha kesi hiyo kuwa ya dharura na kuagiza pande zote kusubiri majaji watatu wateuliwe kusikiliza rufaa ya kampuni hiyo.

Kampuni inasema kwamba akaunti ya benki iliyotuma pesa hizo ni ya kampuni ya Mawakili ya Amadi and Associates na ilifunguliwa na Bi Amadi baada ya kujiunga na Mahakama.

  • Tags

You can share this post!

KRA yaondolea Kidero kesi ya ushuru wa Sh427 milioni

Mabilioni yamwagika kukabili mabadiliko ya tabianchi Afrika

T L