• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 4:54 PM
Kanisa laomba usalama uimarishwe msimu wa sherehe

Kanisa laomba usalama uimarishwe msimu wa sherehe

Na SAMMY KIMATU

KANISA limeomba walinda usalama wawe chonjo msimu wa sherehe na shughuli nyingi ili kuhakikisha Wakenya wanakaa katika mazingira salama.

Hayo yalinenwa Jumapili na askofu mkuu wa kanisa la Baraka, Mathews Nyende Oduori.

Alisema hayo wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa hilo katika mtaa wa mabanda wa Kibera katika kaunti ndogo ya Kibra.

Aidha, Bw Nyende aliongeza kwamba ni bora serikali kuwalinda abiria ili wasitozwe nauli ya juu na wenye matatu.

“Ni mtindo wa kawaida kwa wahudumu wa usafiri wa umma kupandisha nauli tunapokaribia Krismasi hivyo kuna umuhimu wa serikali kuwalinda wananchi wasitozwe ada ya juu,” askofu Nyende akanena.

Vilevile, aliwasihi waumini kuepuka kukusanyika makundi makubwa na kuongeza kwamba ni sharti wadumishe maagizo ya wizara ya afya ya kujikinga dhidi ya msambao wa corona.

Kuhusu madhabahu, alisema wanasiasa wasiruhusiwe kuhutubia kanisa wakisimama mahali hapo akifafanua kuwa ni patakatifu kwa mujibu wa mafunzo ya Biblia.

“Yeyote anayesimama mbele kwa madhabahu kanisani sharti awe ametakazwa kwa kupakwa mafuta. Sio kila mtu anakubaliwa kusimama eneo hilo kanisani,” askofu Nyende akasema.

You can share this post!

Majonzi zaidi ya 30 wakihofiwa kufariki mtoni

Real Madrid wacharaza Sociedad na kufungua pengo la alama...

T L