• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
Kichuna Huddah Monroe asema Ruto atakuwa rais mbovu zaidi katika historia ya Kenya

Kichuna Huddah Monroe asema Ruto atakuwa rais mbovu zaidi katika historia ya Kenya

Na MWANDISHI WETU

SOSHOLAITI Huddah Monroe amedai kuwa Rais William Ruto atakuwa rais mbovu zaidi katika historia ya Kenya.

Monroe alitoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram siku chache baada ya Mamlaka ya Kusimamia Sekta ya Kawi na Petroli (EPRA) kuongeza bei ya mafuta nchini.

Wiki jana, bei ya mafuta ilipoongezwa, petroli ilipanda kwa Sh16.9 kwa lita, dizeli kwa Sh21.31 huku bei ya mafuta taa ikipaa kwa Sh33.22 kwa lita.

Bei hii mpya ilipandisha petroli kuwa Sh211.64 kwa lita jijini Nairobi huku dizeli ikiuzwa kwa Sh200.9 kwa lita na mafuta taa yakiuzwa kwa Sh202.6 kwa lita kuanzia Septemba 14 usiku wa manane.

Jumbe alizochapisha Huddah kwenye Instagram. Picha|Hisani

“Kenya itarudi nyuma kwa miaka 30 sababu pesa zote zinafunganywa na kusafirishwa nje ya nchi. Mabaya zaidi bado hayajakuja,” akaandika.

Isitoshe, Monroe alisema kuwa amejifunza kuwa katu hatawahi kumchagua rais anayetoka katika familia ya uchochole.

Rais Ruto alilelewa na wazazi maskini huku maisha yake ya utotoni yakigubikwa na shida, kulinga na simulizi zake. Hapo awali, Rais Ruto alisema kuwa alitembea mguu chuma shuleni na kuvalia viatu kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 15.

“Niliuza kuku na njugu karanga barabarani eneo la Bonde la Ufa,” aliwahi kunukuliwa.

Hata hivyo, hapo awali, Monroe amekuwa akimpigia debe na kumshabikia Rais Ruto huku akisema kuwa ni kiongozi mwenye maono mazuri ya nchi.

“Ruto atasalia rais mwenye ujasiri. Anaangazia maendeleo ya nchi kwa miaka 10-20. Familia zinazoishi barabarani wanaangazia tu chakula cha mchana na jioni. Hatuwezi tukashinda hivyo. Maskini watasalia maskini na matajiri watabaki matajiri,” aliwahi kuandika.

  • Tags

You can share this post!

Eneobunge lisilo na hata inchi moja ya lami tangu uhuru

Serikali yatafuta Sh162 bilioni za matumizi miezi miwili tu...

T L