• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 7:02 PM
Kinara wa KNUT amrukia Sossion kuhusu zogo

Kinara wa KNUT amrukia Sossion kuhusu zogo

Na FAITH NYAMAI

KATIBU Mkuu wa Chama cha Kitaifa cha Walimu (Knut), Collins Oyuu amelaumu mtangulizi wake Wilson Sossion kwa kuchochea mizozo ndani ya chama hicho.

Bw Oyuu amelaumu kundi linaloongozwa na Bi Martha Omollo, chini ya mwavuli wa “Teachers Pressure Group” kwa kutumiwa na Bw Sossion kuvuruga Knut.

“Ikiwa anataka kuwakilisha walimu, asubiri hadi uchaguzi ujao kugombea wadhifa,” Bw Oyuu alisema.

Bi Omollo na Bw Sossion walikanusha madai ya Bw Oyuu.

Bw Oyuu alisema kwamba hatakubali yeyote kuingilia usimamizi wa Knut.

“Kwa wakati huu mimi ndiye katibu mkuu wa Knut na nimepewa nguvu na walimu kujadili na kuzungumza kwa niaba yao, hivyo mtu mwingine yeyote anayedai kuzungumza kwa niaba ya walimu anafaa kufahamu kuwa hatafaulu,” alisema Bw Oyuu.

Alisema licha ya Bw Sossion kujiondoa katika uchaguzi uliofanyika Juni, ameendelea kutumia makundi mengine kuvuruga juhudi za maafisa wapya wa Knut kufufua chama. hicho.

“Walimu hao, wanaongozwa na Martha, wanaongozwa na Sossion, wanachosoma katika taarifa zao kwa wahababari kinaandikwa na Sossion. Hao ni wabinafsi na hawaendi popote,” alisema Bw Oyuu.

Bw Sossion alipuuza madai ya Bw Oyuu na kusema aliondoka Knut na hafai kuhusishwa na masuala ya chama hicho.

Mbunge Maalum Wilson Sossion. Picha/ Maktaba

Bi Omollo pia alikanusha kwamba anatumiwa na Bw Sossion.

You can share this post!

Amri watumishi wa umma wafichue mali zao

Serikali imeshindwa kukabili ukame – Ripoti

T L