• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 6:55 PM
King’ara asambaza viti vya magurudumu Githurai kwa watoto wenye mahitaji

King’ara asambaza viti vya magurudumu Githurai kwa watoto wenye mahitaji

Na SAMMY WAWERU

MBUNGE wa Ruiru Bw Simon King’ara ameendeleza mradi wake wa usambazaji wa viti vya magudurudumu kwa wakazi wenye matatizo ya kutembea katika eneobunge hilo.

Chini ya Wakfu wa Simon Ng’ang’a King’ara, mbunge huyo amekuwa akisaidia wenye ulemavu eneo la Ruiru.

Mnamo Alhamisi jioni, Bw King’ara alisambaza viti vitano vya magudurumu kwa watoto wenye ulemavu eneo la Githurai 45.

Mtaa wa Githurai 45 uko katika eneobunge la Ruiru, Kaunti ya Kiambu.

“Mbali na kutekeleza miradi mingine ya maendeleo, ni muhimu kama kiongozi kuwapiga jeki wasiojiweza,” Bw King’ara akasema.

“Nimekuwa nikisambaza viti vya magurudumu kwa wenye matatizo ya kutembea eneobunge la Ruiru, na pia kuwapa misaada kutatua mahitaji muhimu ya kimsingi,” mbunge huyo akaambia Taifa Jumapili.

Mbunge wa Ruiru Bw Simon King’ara (mwenye suti ya bluu) alisambaza viti vya magurudumu kwa watoto wenye matatizo ya kutembea eneo la Githurai. Picha/ Sammy Waweru

Hafla ya usambazaji wa viti vya magurudumu eneo la Githurai iliandaliwa katika afisa za D.O eneo la Githurai, Ruiru.

Mbali na kulenga wenye mahitaji maalum katika jamii, Bw King’ara amekuwa akitumia wakfu huo kutoa hamasisho kwa vijana kuhusu chaguo bora la kazi, kupambana na dawa za kulevya na mimba za mapema.

Katika usambazaji wa viti vya magurudumu eneo la Githurai, mbunge huyo pia alitoa hundi la Sh20, 000 kusaidia watoto waliofaidika.

You can share this post!

JAMVI: Joho na Kingi waanza kumkama Raila kijasho

Shujaa, Lionesses wala rungu kali fainali ya Madrid Sevens