• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Kiongozi wa kijeshi Guinea aapishwa kuwa rais wa mpito

Kiongozi wa kijeshi Guinea aapishwa kuwa rais wa mpito

Na MASHIRIKA

CONAKRY, Guinea

Tafsiri: CHARLES WASONGA

KIONGOZI wa kijeshi nchini Guinea Mamadi Doumbouya Ijumaa aliapishwa kuwa Rais wa mpito nchini humo baada ya kung’olewa mamlakani kwa Rais Alpha Conde.

Sherehe ya kuapishwa kwake ilifanyika katika Kasri ya Mohamed VI jijini Conakry na haikuhudhuriwa na viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi.Mwezi jana, marais wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) waliwawekea viongozi hao wa kijeshi pamoja na jamaa zao.

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, kumtokea mapinduzi manne ya kijeshi katika mataifa ya Magharibi na Kati mwa Afrika. Misukosuko ya kisiasa imechangia mataifa ya ukanda huo wa Afrika kutumbukia katika mapinduzi ya kijeshi na kusababishia raia ufukara.

Hii ni licha ya kwamba eneo hilo lina utajiri mkubwa wa rasilimali haswa madini. Huku akiwa amevalia sare za kijeshi, kofia nyekundu na miwano, Kanali Doumbouya aliinua mkono na kula kiapo.

“Ninatambua wajibu mkubwa ambao umewekwa kwangu,” akasema katika hotuba fupili. Doumbouya aliahidi kusimamia kipindi cha mpito ambacho kitajumuisha kuandikiwa kwa katiba mpya, kupambana na ufisadi, mageuzi ya sheria za uchaguzi na utayarishaji wa uchaguzi mkuu ulio huru

Mwanajeshi huyo alisema kuwa wanachama wa serikali yake ya mpito watazuiwa kuwania nyadhifa za uongozi katika uchaguzi mku ujao. Hata hivyo, hakudokeza ni lini uchaguzi huo utafanyika.

Hata hivyo,  Doumbouya alisema tarehe ya uchaguzi huo itaaamuliwa na Baraza la Kitaifa la Mpito lenye wanachama 81. Viongozi wa kijeshi wanasema walimwondoa mamlakani Conde kutokana na malalamishi ya wananchi kutokana na kukithiri kwa umasikini, ufisadi na uongozi mbaya nchini humo.

  • Tags

You can share this post!

Pele aondoka hospitalini na kurejea nyumbani baada ya...

Wachezaji wa Brighton na Southampton katika kikosi cha Mali...