• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 5:59 PM
Kocha David Moyes arefusha kandarasi yake kambini mwa West Ham kwa miaka mitatu

Kocha David Moyes arefusha kandarasi yake kambini mwa West Ham kwa miaka mitatu

Na MASHIRIKA

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

KOCHA David Moyes, 58, amerefusha mkataba wake kambini mwa West Ham United kwa kipindi cha miaka mitatu zaidi.

Katika awamu yake ya pili ya ukocha ugani London Stadium, mkufunzi huyo raia wa Scotland aliowaongoza West Ham kukamilisha kampeni za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) katika nafasi ya sita kwa alama 65 ambazo ni za juu zaidi kwa kikosi hicho kuwahi kujivunia katika historia.

Mafanikio hayo ya Moyes yaliwapa West Ham tiketi ya kunogesha kampeni za Europa League mnamo 2021-22.“Nina furaha kwamba nimerefusha muda wa kuhudumu kwangu kambini mwa West Ham,” akasema Moyes ambaye pia amewahi kudhibiti mikoba ya Everton, Manchester United na Preston North End.

Moyes alirejea kuwatia makali vijana wa West Ham mnamo Disemba 2019 baada ya mkufunzi raia wa Chile, Manuel Pellegrini kuondoka.

Moyes aliwahi kuwaongoza West Ham kwenye EPL kwa kipindi cha miezi saba kuanzia Novemba 2017 na alikuwa akihusishwa pakubwa na uwezekano wa kurejea Everton wanaotafuta kizibo cha Carlo Ancelotti aliyerejea Real Madrid ya Uhispania mnamo Mei 2021.

Moyes amewahi pia kuwatia makali vijana wa Sunderland na Real Sociedad. Hadi sasa, anajivunia kusimamia jumla ya mechi 583 za EPL na anashikilia nafasi ya nne nyuma Sir Alex Ferguson, Arsene Wenger na Harry Redknapp kwenye orodha ya wakufunzi ambao wanajivunia kusimamia idadi kubwa zaidi ya michuano ya EPL.

  • Tags

You can share this post!

Ubelgiji na Finland wakung’uta Urusi na Denmark...

Wahudumu walia kuhusu ada mpya za tuk tuk